Wananchi wa Iran wafanya maandamano kulaani jinai za Israel dhidi ya Wapalestina
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i44664-wananchi_wa_iran_wafanya_maandamano_kulaani_jinai_za_israel_dhidi_ya_wapalestina
Wananchi wa Iran wamemiminika mabarabarani baada ya Sala ya Ijumaa hii leo kushiriki maandamanao ya kulaani vikali jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina, sambamba na uamuzi wa upande mmoja wa Marekani wa kuuhamishia ubalozi katika mji mtukufu wa Quds, kutoka Tel Aviv.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 18, 2018 10:15 UTC
  • Wananchi wa Iran wafanya maandamano kulaani jinai za Israel dhidi ya Wapalestina

Wananchi wa Iran wamemiminika mabarabarani baada ya Sala ya Ijumaa hii leo kushiriki maandamanao ya kulaani vikali jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina, sambamba na uamuzi wa upande mmoja wa Marekani wa kuuhamishia ubalozi katika mji mtukufu wa Quds, kutoka Tel Aviv.

Maandamano hayo yameshuhudiwa katika miji na mikoa mbalimbali ya Iran, ambapo waandamanaji licha ya makali ya saumu ya Ramadhani wamesikika wakipiga nara za kuulaani utawala haramu wa Israel kwa kufanya mauaji ya umati dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Nakba, iliyosadifiana na siku ambayo Marekani ilikuwa inauhamishia ubalozi wake mjini Quds.

Huku wakiwa wamebeba bendera za Palestina, maelfu ya waandamanaji hao wa Kiirani wamesikika wakisema, "Mauti kwa Marekani", 'Mauti kwa Israel", "Mauti kwa Uingereza", na "Mauti kwa Aal-Saudi".

Waislamu wakiandamana huko Pakistan

 

Waandamanaji hao wamesikika wakikosoa vikali kimya cha jamii ya kimataifa mbele ya jinai hizo za kuogofya za utawala katili wa Israel dhidi ya Wapalestina madhulumu.

Mataifa mbali mbali ya Kiislamu hii leo baada ya Sala ya Ijumaa yameshuhudia maandamano makubwa ya kulaani ukatili huo wa Israel dhidi ya Wapalestina, na chokochoko za Marekani za kuuhamishia ubalozi wake mjini Quds Tukufu kutoka Tel Aviv.