Rais Rouhani: Iran iko tayari kupanua ushirikiano wa kiuchumi kieneo na kimataifa
(last modified Sun, 10 Jun 2018 08:01:22 GMT )
Jun 10, 2018 08:01 UTC
  • Rais Rouhani: Iran iko tayari kupanua ushirikiano wa kiuchumi kieneo na kimataifa

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran ni mshirika huru na wa kuaminika na iko tayari kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kieneo na kimataifa.

Rais Rouhani amesema hayo leo katika hotuba yake mbele ya kikao cha 18 cha viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai kinachofanyika huko Qingdao nchini China na huku akisisitiza kwamba, inabidi eneo lenye amani zaidi, utulivu zaidi, ustawi zaidi na maendeleo makubwa zaidi liandaliwe mikakati na manufaa ya pamoja ya muda mrefu chini ya msingi wa kuvumiliana kieneo. Ameongeza kuwa, vikwazo vya upande mmoja vinatia doa mchakato wa biashara ya kimataifa na ni jambo lisilo na shaka kwamba fikra ya kujikumbizia upande mmoja masuala yote ya kiuchumi, kisiasa na kisheria inadhoofisha fikra ya ushirikiano wa kieneo.

Ndani ya ukumbi wa kikao cha Shanghai

 

Ameongeza kuwa, njama za Marekani za kujaribu kuyatwisha mataifa ya dunia siasa zake ni hatari kubwa inazidi kuwa kubwa na ni mfano wa karibuni kabisa wa fikra ya kujikumbizia kila kitu upande wake sambamba na msimamo wa Marekani ya kutojali sheria za kimataifa na uamuzi wake wa kijuba wa kujitoa katika mapatano ya kimataifa ya JCPOA.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vile vile amesema, ugaidi, fikra ya kujiteka na misimamo ya kufurutu ada yameathiri vibaya maeneo tofauti duniani na hususan maeneo ya Asia ya Kati na Asia Magharibi na kuongeza kuwa, makundi ya kigaidi yanatumia vibaya elimu ndogo katika nchi za eneo hili na kuvutia watu wengi kujiunga nao.  

Tags