Rais Rouhani: Iran inanyoosha mkono wa udugu kwa Waislamu wote
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i49762-rais_rouhani_iran_inanyoosha_mkono_wa_udugu_kwa_waislamu_wote
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Iran inanyoosha mkono wa udugu kwa Waislamu wote duniani.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 26, 2018 04:34 UTC
  • Rais Rouhani: Iran inanyoosha mkono wa udugu kwa Waislamu wote

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Iran inanyoosha mkono wa udugu kwa Waislamu wote duniani.

Rais Rouhani aliyasema hayo jana mbele ya hadhara ya mabalozi wa nchi za Kiislamu, wasoni na wanafikra wanaoshiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa 32 mjini Tehran waliokwenda kuonana na Kiongozi Muadhamu na kuongeza kuwa, maadui wanataka Iran iwe na mwenendo ule ule wa kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini na isiwatetee watu wanaodhulumiwa, lakini Jamhuri ya Kiislamu inayomfuata Mtume Muhammad (saw) haiogopi matakfiri na madola ya kibeberu.

Rais wa Rouhani amesisitiza kuwa, Iran inawatambua majirani zake kuwa ni ndugu na kwamba, usalama na amani ya eneo hili ni amani na usalama wake na kusisitiza kuwa, njama za madola ya kibeberu za kutaka kuvuruga usalama wa Mashariki ya Kati kwa kutumia vibaraka wao wa kitakfiri na kulishinikiza taifa kubwa la Iran kwa kutumia vikwazo zitafeli na kushindwa. Amesema kuwa, wabaguzi wanaendelea kuwaua kwa umati raia wa Palestina kila siku ya kuwashambulia kwa mabomu raia wa Yemen. 

Vilevile ameashiria ushirikiano uliopo baina ya makundi yenye misimamo mikali ya Kikristo, Kiyahudi na baadhi ya Waislamu na kusema kuwa, Hii leo baadhi ya watu wanaotumia nara ya kukufurisha Waislamu wenzao wamechafua usalama wa jamii na eneo zima la Mashariki ya Kati kwa kutumia jina la Uislamu na Qur'ani na kuangamiza roho za watu, usalama na turathi za ustaarabu. 

Rais wa Iran amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu inataka kuwepo umoja na mshikamano, upendo na hemima na kudumishwa maadili ambavyo haviwezi kupatikana isipokuwa chini ya mwavuli wa Mtume wa Uislamu, Muhammad (saw).