Gazeti la Marekani: Jeshi la IRGC la Iran ni jinamizi kwa Trump
Gazeti la National Interest linalochapishwa nchini Marekani limelielezea Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) kuwa ni jinamizi kubwa zaidi kwa rais wa Marekani Donald Trump.
Gazeti hilo limeashiria hatua ya Ikulu ya rais wa Marekani White House ya kuliweka jeshi hilo kwenye orodha eti ya makundi ya kigaidi na kuandika kuwa, ushawishi na satua ya jeshi hilo la vikosi vya ulinzi vya Iran unapindukia zaidi ya uwezo wa kijeshi.
Gazeti hilo la Marekani limekitaja kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuwa ni ngome imara ya kukabiliana na maslahi ya Marekani katika eneo la Magharibi ya Asia.
National Interest limeongeza kuwa, mbinu tofauti za kijeshi zinazotumiwa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu zimeweza kutoa upinzani na changamoto kwa Marekani.
Itakumbukuwa kuwa siku ya tarehe 20 Juni ndege ya kijasusi isiyo na rubani ya Marekani aina ya Global Hawk ilitunguliwa na kuteketezwa na kikosi cha anga za mbali cha IRGC baada ya kuvuka mpaka wa anga ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Maafisa wa Jamhuri ya Kiislamu wametangaza kuwa kuangushwa kwa droni hiyo ya kisasa kabisa ya Marekani ni jibu kali na la wazi kwa uchokozi wa aina yoyote itakaojaribu kuufanya Washingtin dhidi ya ardhi ya Iran.../