Mousavi: Matamshi ya uhasama hayafiki popote
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i55807-mousavi_matamshi_ya_uhasama_hayafiki_popote
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa matamshi ya uhasama ya Brian Hook Mjumbe Maalumu wa Marekani katika masuala ya Iran hayatafika popote.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 05, 2019 02:51 UTC
  • Mousavi: Matamshi ya uhasama hayafiki popote

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa matamshi ya uhasama ya Brian Hook Mjumbe Maalumu wa Marekani katika masuala ya Iran hayatafika popote.

Sayyid Abbas Araqchi jana usiku alijibu matamshi ya Brian Hook na ugaidi mpya wa kiuchumi unaofanywa na Marekani dhidi ya taifa la Iran na kueleza kuwa: Kushtadi matamshi ya uhasama ni hatua ya kukata tamaa; na ya dhihaka kuliko yote ni kuainishwa tuzo kwa ajili ya jinai na ujasusi kwa lengo la kuwachochea wananchi wa Iran. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa: Mienendo kama hii ya Marekani itazidisha kurasa chafu katika utendaji mbovu wa viongozi wa nchi hiyo mkabala na Iran; viongozi ambao siku moja watapasa kuwajibika kwa vitendo vyao hivyo. Brian Hook Mjumbe Maalumu wa Marekani katika masuala ya Iran alisema mbele ya waandishi habari jana Jumatano kwamba, Iran imewekewa vikwazo vipya na vingine zaidi viko njiani. Hook ambaye amedhihirisha uhasama wa Marekani dhidi ya Iran amesisitiza kwa mara nyingine tena kuwa Marekani imeazimia kuiwekea Iran mashinikizo zaidi na hakuna misamaha yoyote iliyoko kwenye ajenda yake ya kazi. 

Brian Hook, Mjumbe Maalumu wa Marekani katika masuala ya Iran