Rabii: Iran inaendeleza juhudi zake za kuimarisha amani na urafiki katika eneo
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i56481-rabii_iran_inaendeleza_juhudi_zake_za_kuimarisha_amani_na_urafiki_katika_eneo
Msemaji wa serikali ya Iran amesisitiza kuwa wale wanaotaka mabaya wafahamu kuwa Iran haitasitisha jitihaa zake za kuendeleza amani na urafiki na majirani zake.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Oct 08, 2019 01:05 UTC
  • Rabii: Iran inaendeleza juhudi zake za kuimarisha amani na urafiki katika eneo

Msemaji wa serikali ya Iran amesisitiza kuwa wale wanaotaka mabaya wafahamu kuwa Iran haitasitisha jitihaa zake za kuendeleza amani na urafiki na majirani zake.

Ali Rabii jana aliashiria katika kikao na waandishi wa habari kuhusu njama za maadui kwa lengo za kuvuriga uhusiano kati ya Tehran na majirani zake na kueleza kuwa nchi za eneo la Ghuba ya uajemi zinapasa kuwa macho na njama hizo za maadui.

Rabii aliongeza kusema kuwa lengo la Iran ni kuimarisha uhusiano na nchi zote za eneo na jirani na khususan nchi za Ghuba ya Uajemi. Msemaji wa serikali ya Iran aidha ameeleza kusikitishwa na matuki ya siku kadhaa zilizopita huko Iraq na kueleza kuwa: Iran inatiwa wasiwasi na machafuko ya aina yoyote na mivutano katika nchi jirani na inataka kufanyika jitihada za dhati ili kulinda uthabiti katika nchi zote za eneo. Msemaji wa serikali ya Iran ameongeza kuwa kama ilivyo siku zote, Iran iko tayari kuwa pamoja na bega kwa bega na wananchi wa Iraq na kutoa kila aina ya msaada kwa wananchi hao. Amesema propaganda bandia na sumu hazitafanikiwa kuyatenganisha mataifa haya mawili.