Rais Rouhani: Iran imevibadilisha vikwazo na kuvifanya kuwa fursa
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria vikwazo vya kidhalimu vya Marekani dhidi ya wananchi wa taifa hili na kusema kuwa, Tehran imesimama kidete na kuvibadilisha vikwazo na mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa ya maadui na kuwa fursa.
Rais Rouhani aliyeko Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano wa Kuala Lumpur amesema hayo leo alipokutana na Wairani wanaoishi nchini humo na kueleza kwamba, wananchi wa Iran wamesimama kidete mbele ya vikwazo vya kidhalimu vya Marekani ambayo vimejumuisha pia bidhaa za chakula na dawa.
Rais Rouhani amesema kuwa, Marekani na Wazayuni wameiwekea vikwazo na mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa Iran lengo lao lilikuwa ni kutoa pigo dhidi ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.
Rais wa Iran kadhalika amesema kwamba, kiwango cha taifa hili cha kukabiliana na mashinikizo ya kigeni ni kikubwa ikilinganishwa na huko.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameiponda njia iliyochagua Marekani ya kutumia vikwazo kama wenzo wa kufikia malengo yake na kusema kuwa, watu wote wanatambua vyema kwamba, kujitoa Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA hakuna maslahi na yeyote hata Washington na marafiki zake.
Aidha amesema, taifa la Iran daima limekuwa likipinga vitendo vya utumiaji mabavu na ugaidi na kuongeza kwamba, ujumbe wa Iran ni kuweko uhusiano na ushirikiano katika nyanja zote baina ya mataifa yote ya dunia hususan nchi za Kiislamu