Rouhani: Iran inafadhilisha kuwa na uhusiano mzuri na nchi za Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i6334-rouhani_iran_inafadhilisha_kuwa_na_uhusiano_mzuri_na_nchi_za_afrika
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema taifa hili linafadhilisha kuwa na mahusiano mazuri na nchi za Afrika ikiwemo Togo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 03, 2016 23:36 UTC
  • Rouhani: Iran inafadhilisha kuwa na uhusiano mzuri na nchi za Afrika

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema taifa hili linafadhilisha kuwa na mahusiano mazuri na nchi za Afrika ikiwemo Togo.

Rais Rouhani aliyasema hayo Jumanne baada ya kumpokea rasmi balozi mpya wa Togo mjini Tehran Mohamed Sad Ouro-Sama. Alisema daima Tehran iko tayari kuimarisha ushirikiano wake na nchi za Afrika katika nyuga tofauti.

Rais Hassan Rouhani wa Iran ameelezea utayarifu wa Tehran kuimarisha ushirikiano na uhusiano wake na Lome katika nyuga za uchumi, utamaduni na siasa.

Kadhalika Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa wito wa kushirikina nchi hii na Togo katika vita dhidi ya ugaidi sambamba na kuyapatia ufumbuzi matatizo ya kieneo na kimataifa.

Kwa upande wake, Mohamed Sad Ouro-Sama, balozi mpya wa Togo mjini Tehran amepongeza juhudi za Iran za kuleta amani na uthabiti katika eneo hili la Mashariki ya Kati sanjari na kupambana na ugaidi.

Aidha ametoa wito wa kuimarishwa uhusiano katika nyuga mbai mbali kati ya Iran na nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Rais Hassan Rouhani amekuwa akisisitiza kuwa, suala la Iran kuimarisha ushirikiano na nchi za bara la Afrika ni katika ajenda kuu ya sera za kigeni za Jamhuri ya Kiislamu.