Khatibzadeh: Wairani hawatishwi na matusi na bwabwaja za Trump
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i63928-khatibzadeh_wairani_hawatishwi_na_matusi_na_bwabwaja_za_trump
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran mapema leo amejibu matamshi ya kifidhuli yaliyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kusema kuwa, wananchi wa Iran hawatishwi na matusi na maneno ya kibabe ya utawala uliofeli wa Marekani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 09, 2020 23:45 UTC
  • Saeed Khatibzadeh
    Saeed Khatibzadeh

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran mapema leo amejibu matamshi ya kifidhuli yaliyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kusema kuwa, wananchi wa Iran hawatishwi na matusi na maneno ya kibabe ya utawala uliofeli wa Marekani.

Saeed Khatibzadeh ameandika leo katika mtandao wa Twitter kwamba Wairani hawatishiki kwa bwabwaja za utawala uliofeli na usio na faida wa Marekani na kwamba wananchi wa Irani ndio watakaochagua jibu mwafaka dhidi ya jinai za Marekani vikiwemo vikwazo vya kiendawazimu na mauaji yaliyofanywa na utawala wa Trump dhidi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliyekuwa adui nambari moja wa kundi la kigaidi la Daesh. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, Wairani hawatasita kufanya lolote kwa ajili ya kulinda heshima na hadhi yao. 

Rais Donald Trump wa Marekani Ijumaa ya jana alifanya mahojiano na redio moja ya nchi hiyo na kutoa tena vitisho dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kutumia matusi na maneno ya kifidhuli. 

Trump alidai katika mahojiano yake na Rush Limbaugh kwamba serikali yake imetoa tahadhari kali kwa Iran isichukue hatua yoyote dhidi ya Marekani. 

Donald Trump

Utumiaji wa matusi na maneno ya kijuba katika mahojiano hayo umedhihirisha tena chuki kubwa na kufeli kwa sera za mashinikizo ya kiwango cha juu za serikali ya Trump dhidi ya taifa la Iran.

Baada ya kurushwa hewani mahojiano hayo vyombo vya habari na wanaharakati wa Marekani wamemtaja Donald Trump kuwa ni mtu mwenye "mdomo mchafu".

Kiongozi huyo amekuwa akitoa bwabwaja na vitisho vya mara kwa mara kutokana na woga wa kisasi kikali cha Jamhuri ya Kiislamu dhidi ya mauaji ya aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Luteni Jenerali Qassem Soleimani yaliyofanywa na jeshi la magaidi wa Marekani.  

Kamanda Soleimani na wenzake kadhaa waliuawa na jeshi la kigaidi la Marekani Ijumaa ya tarehe 3 Januari mwaka huu katika shambulizi la anga lililolenga gari lake karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq. Jenerali Soleimani alikuwa safarini nchini humo kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa Iraq.