Rais Rouhani: Wasiovaa barakoa Tehran kutozwa faini
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i63938-rais_rouhani_wasiovaa_barakoa_tehran_kutozwa_faini
Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema watakaopatikana na hatia ya kutovaa barakoa mjini Tehran watatozwa faini riali laki tano
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 10, 2020 08:36 UTC
  • Rais Rouhani: Wasiovaa barakoa Tehran kutozwa faini

Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema watakaopatikana na hatia ya kutovaa barakoa mjini Tehran watatozwa faini riali laki tano

Rais Rouhani ameyasema hayo leo mjini Tehran wakati wa kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na Corona ambapo ametangaza hatua kadhaa zitakazochukuliwa kukabiliana na janga la corona. Rais Rouhani amesema watakaokuwa na jukumu la kutekeleza sheria ya kuhakikisha wote wanavaa barakoa ni Jeshi la Polisi na Jeshi la Kujitolea la Wananchi (Basiji). Aidha kila atakayekiuka sheria ya kukaa katika karantini atatozwa faini ya riali milioni mbili.

Rais Rouhani amesema sheria hiyo ya barakao na karantini inahusiana na mji wa Tehran kwa sasa na kuongeza kuwa iwapo, itahitajika sheria hiyo inaweza pia kutumiwa katika miji mingine ya Iran. Hali kadhalika amesema Iran imetanga dola milioni 100 kununua vifaa vya kupima corona kutoka nchi za kigeni na kwa msingi huo kutakuwa na mabadiliko makubwa katika vipimo hivyo hivi karibuni.

Rais wa Iran ameashiria wimbi jipya la maambukizi ya corona duniani na kusema hali hii imejitokeza kutokana na upuuzaji wa misingi ya kiafya.