Kiongozi Muadhamu awatakia kheri Wakristo katika sherehe zao za X-Mass
(last modified Sat, 26 Dec 2020 02:57:44 GMT )
Dec 26, 2020 02:57 UTC
  • Kiongozi Muadhamu awatakia kheri Wakristo katika sherehe zao za X-Mass

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewatumia ujumbe Wakristo wa Iran na duniani kwa ujumla akiwatakia kheri katika sherehe zao wa X-Mass.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran Press, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema katika ujumbe wake kupitia Twitter na ambao ameutuma kwa lugha ya Kiingereza kwamba, anawatakia kheri Wakristo wa Iran na duniani kiujumla katika sherehe zao za kukumbuka kuzaliwa Nabii Isa mwana wa Maryam AS.

Ujumbe huo umesema, ninatoa mkono wa baraka kwa Wakristo na Waislamu kote duniani na hasa raia wenzangu wa Iran wa dini ya Kikristo kwa mnasaba wa maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Nabii Isa AS.

Wakristo duniani, jana Ijumaa waliadhimisha sikukuu yao ya X-Mass wanayoinasibisha na siku ya kuzaliwa Nabii Isa mwana wa Maryam AS, sherehe ambazo hufanyika tarehe 25 Disemba kila mwaka.