Wasomi wa Iran na Russia: Ubeberu wa Marekani unaelekea ukingoni
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i66776-wasomi_wa_iran_na_russia_ubeberu_wa_marekani_unaelekea_ukingoni
Kundi la wasomi na wanafikra wa Russia na Iran walioshiriki katika mkutano uliopewa anwani ya "Kuporomoka Marekani, Taathira za Mapinduzi ya Kiislamu katika Kanda ya Asia na Duniani", wamechunguza taathira za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ulimwenguni na kusisitiza kwa pamoja kwamba, umri wa ubeberu wa Marekani unaelekea ukingoni na mwenendo wa kuporomoka kwake umefikia katika nukta ya kutorejea nyuma.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 12, 2021 08:48 UTC
  • Wasomi wa Iran na Russia: Ubeberu wa Marekani unaelekea ukingoni

Kundi la wasomi na wanafikra wa Russia na Iran walioshiriki katika mkutano uliopewa anwani ya "Kuporomoka Marekani, Taathira za Mapinduzi ya Kiislamu katika Kanda ya Asia na Duniani", wamechunguza taathira za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ulimwenguni na kusisitiza kwa pamoja kwamba, umri wa ubeberu wa Marekani unaelekea ukingoni na mwenendo wa kuporomoka kwake umefikia katika nukta ya kutorejea nyuma.

Mkutano huo umefanyika leo Ijumaa mjini Moscow ukihudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu wa pande hizo mbili.

Mwakilishi wa Faqihi Mtawala nchini Russia, Hujjatul Islam Saber Akbari Jeddi amesema mwanzoni mwa mkutano huo kwamba, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yamekuwa na taathira kubwa kwa masuala ya kikanda na kimataifa na kwa kambi mbili za Mashariki na Magharibi. 

Akbari Jeddi amesema kuwa, kutokea kwa Mapinduzi ya Kiislamu ulikuwa mwanzo wa kuporomoka kambi mbili za Mashariki na Magharibi ambazo zilikuwa zikikabiliana, na kusisitiza kuwa Mapinduzi hayo pia yalikuwa mwanzo wa kusambaratika madola makubwa ya kibeberu na yanayozozana.

Baadhi ya washirika katika mkutano wa Moscow

Kwa upande wake, balozi wa Iran mjini Moscow Kazem Jalali ambaye pia amehutubia mkutano huo amesema Jamhuri ya Kiislamu imeendelea kusimama kidete dhidi ya utawala wa kibebeberu wa Marekani. Ameongeza kuwa, mwaka 2000 Russia pia iliingia katika medani hiyo na kukabiliana na sera za kujichukilia maamuzi ya upande mmoja za utawala wa kibeberu wa Marekani huku China ikigeuka na kuwa nguvu kubwa ya kiuchumi. Balozi Jalali amesisitiza kuwa hali hiyo ilitoa changamoto kubwa kwa utawala wa Marekani.

Mwanasiasa mashuhuri wa Russia, Sergey Baburin ambaye aligombea kiti cha rais wa nchi hiyo mwaka 2018 pia amesema katika mkutano huo kwamba, Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979 nchini Iran yaliirejesha jamii ya mwanadamu katika masuala ya kiroho na maadili mema.