Brigedia Jenerali Dehqan: Uwezo wa kiulinzi wa Iran hautegemei silaha za nyuklia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i67236-brigedia_jenerali_dehqan_uwezo_wa_kiulinzi_wa_iran_hautegemei_silaha_za_nyuklia
Mshauri wa Amirijeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran katika masuala ya sekta ya viwanda vya ulinzi amezungumzia fatwa ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu juu ya kuwa haramu kuunda na kutumia silaha za nyuklia na kusisitiza kuwa, uwezo wa kiulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katu hautegemea na hautategemea silaha za nyuklia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 25, 2021 00:22 UTC
  • Brigedia Jenerali Dehqan: Uwezo wa kiulinzi wa Iran hautegemei silaha za nyuklia

Mshauri wa Amirijeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran katika masuala ya sekta ya viwanda vya ulinzi amezungumzia fatwa ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu juu ya kuwa haramu kuunda na kutumia silaha za nyuklia na kusisitiza kuwa, uwezo wa kiulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katu hautegemea na hautategemea silaha za nyuklia.

Brigedia Jenerali Hossein Dehqan amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran siku zote imekuwa ikishirikiana na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) na ni miongoni mwa nchi chache duniani zilizosaini mkataba wa NPT na kueleza kuwa: Tehran kamwe haijawahi kuchukua na haitachukua hatua ya kuunda silaha za nyuklia. 

Ameongeza kuwa, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa fatwa ya kidini ya kupiga marufuku silaha za nyuklia na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapinga hatua yoyote ya kuunda, kumiliki na kutumia silaha za maangamizi ya halaiki, hasahasa silaha za nyuklia. 

Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu  

Brigedia Jenerali Dehqan amekumbusha kuwa: Ulimwengu mzima unajua vyema kuwa nchi pekee aliyounda, kumiliki na kutumia bomu la nyuklia ni Marekani na ni dhahir shahir kwamba, vita baridi vilianzishwa ikiwa ni matokeo ya hatua zilizochukuliwa na nchi mbalimbali kuelekea kuunda silaha za nyuklia huku nchi hizo zikizitaja silaha hizo kuwa ni kwa ajili ya kujilinda.