Ujumbe wa Rais wa Russia kwa Kiongozi Muadhamu wakabidhiwa Dkt. Velayati
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i67602-ujumbe_wa_rais_wa_russia_kwa_kiongozi_muadhamu_wakabidhiwa_dkt._velayati
Ujumbe wa Rais Vladimir Putin wa Russia kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, umekabidhiwa kwa Mshauri wa Kiongozi Muadhamu Dkt. Ali Akbar Velayati.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 07, 2021 01:20 UTC
  • Ujumbe wa Rais wa Russia kwa Kiongozi Muadhamu wakabidhiwa Dkt. Velayati

Ujumbe wa Rais Vladimir Putin wa Russia kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, umekabidhiwa kwa Mshauri wa Kiongozi Muadhamu Dkt. Ali Akbar Velayati.

Dkt. Velayati ameupokea rasmi ujumbe huo wa maandishi kutoka kwa Balozi wa Russia nchini Iran Levan Dzhagaryan.

Katika mkutano wa kupokea ujumbe huo, Velayati amesema Iran na Russia ni marafiki muhimu na majirani wenye uthabiti. Amesema uhusiano wa Iran na Russia umejengeka katika msingi wa kuheshimiana,

Dkt. Velayati ameongeza kuwa, matukio ya kieneo na kimataifa yamepelekea kuimarika zaidi uhusiano wa Russia na Iran. Aidha amesema uhusiano wa kistratijia unahitaji kuwepo ushirikiano katika uga wa kimataifa na kieneo na kuongeza kuwa, kwa bahati nzuri ushirikiano baina ya Iran na Russia kuhusu Syria, ambao ulitokana na mwaliko rasmi wa wakuu wa Syria, umesaidia kukabiliana na maadui katika nchi hiyo ya Kiarabu ambao walikuwa wameilazimishia vita vya kimataifa vilivyojumuisha zaidi ya nchi 70.

 Spika wa Bunge la Iran Mohammad Baqer Qalibaf (kushoto) akimkabidhi Spika wa Bunge la Russia Duma Vyacheslav Volodin ujumbe maalumu wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Rais Vladimir Putin wa nchi hiyo

Balozi wa Russia amewasilisha ujumbe huo wa Rais Putin ambao ni jibu kwa ujumbe ambao Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alimtumia rais huyo wa Russia. Ujumbe  wa Kiongozi Muadhamu ulifikishwa Russia na Spika wa Bunge la Iran Mohammad Baqeir Qalibaf mapema mwezi Februari.

Balozi huyo amesema kuiamrishwa uhusiano wa Iran na Russia ni jambo ambalo limepelekea kuimarika ushirikiano wa nchi hizi mbili.