Fainali ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu nchini Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i67642-fainali_ya_mashindano_ya_kimataifa_ya_qur'ani_tukufu_nchini_iran
Fainali ya Mashindano ya 37 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran inaendelea ambapo kuna washiriki kutoka kona zote za dunia.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Mar 08, 2021 00:11 UTC
  • Fainali ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu nchini Iran

Fainali ya Mashindano ya 37 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran inaendelea ambapo kuna washiriki kutoka kona zote za dunia.

Mashindano ya mwaka huu ni ya kipekee kwani kutokana na janga la  COVID-19 au corona, yanafanyika kwa njia ya Intaneti.

Kwa mujibu wa taarifa mashindano hayo yana majaji 23 kutoka Iran na wengine saba kutoka Sudan, Lebanon, Indonesia, Syria, Tunisia na Jordan. Majaji hao ambao wote ni wataalamu wa Qur’ani watasimamia zoezi zima la kusoma na kuhifadhi Qur’ani katika mashindano hayo.

Mtaalamu mkongwe wa Qur’ani kutoka Iran, Ustadh Abbas Salimi anaongoza jopo hilo la majaji katika mashindano hayo ambayo yameanza Machi sita na yanatazamiwa kumalizika Machi 11.

Mashiriki wa mashindano ya Qur'ani kwa njia ya intaneti

Mbali na kufanyika kwa njia ya intaneti, mashindano hayo pia yanarushwa hewani mubashara kupitia Televisheni ya Qur'ani ya IRIB, Radio ya Qur'ani ya IRIB na majukwaa mengine ya mtandaoni.

Kauli mbiu ya mashindano ya mwaka huu ni 'Kitabu Kimoja, Ummah Mmoja".

Zaidi watazamaji milioni 2.5 walifuatilia duru za mchujo za mashindano hayo kwa njia ya intaneti na inatazamiwa kuwa baina ya watu milioni 6-8 watafuatilia fainali ya mashindano hayo kwa njia ya intaneti.