Zarif asisitiza: "Vikwazo vya kulemaza" vya Marekani vimefeli na kugonga mwamba
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i72352-zarif_asisitiza_vikwazo_vya_kulemaza_vya_marekani_vimefeli_na_kugonga_mwamba
Waziri wa Mashauri wa Kigeni wa Iran amesema kuwa vikwao vya Marekani dhidi ya Iran vilivyotajwa kuwa ni vya kulemaza vimefeli na kushindwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 14, 2021 08:02 UTC
  • Dokta Muhammad Javad Zarif
    Dokta Muhammad Javad Zarif

Waziri wa Mashauri wa Kigeni wa Iran amesema kuwa vikwao vya Marekani dhidi ya Iran vilivyotajwa kuwa ni vya kulemaza vimefeli na kushindwa.

Dokta Muhammad Javad Zarif ameyasema hayo leo kwa mnasaba wa kutimia mwaka wa 6 tangu mapatano ya nyuklia ya Iran na mataifa kadhaa yenye nguvuni duniani yalipotiwa saini.

Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa Twitter, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema: Siku kama hii ya leo miaka 6 iliyopita makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yalitatua maudhui muhimu iliyoko kwenye kifungu cha 7 cha hati ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa bila ya kutumia mabavu wala vita.

Muhammad Javad Zafi ameongeza kuwa: Barack Obama alielewa vyema kwamba, "vikwazo vyake eti vya kulemaza" havikuweza kuilemaza Iran wala mashinepewa za kurutubisha madini ya urani hapa nchini; na Trump alidhani kipumbavu, kwamba "mashinikizo ya kiwango cha juu zaidi" yatafuadafu, lakini pia yalishindwa. 

Donald Trump

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema, Rais wa Marekani anapaswa kutazama kwa makini takwimu hizo. 

Makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yalitiwa saini miaka 6 iliyopita baada ya kufikiwa mapatano ya Lausanne, Jumanne, Julai 14, 2015 huko Vienna, Austria kati ya Iran, Umoja wa Ulaya na nchi wanachama katika kundi la 5+1 ambalo lilijumuisha Russia, China, Uingereza, Ufaransa, Marekani pamoja na Ujerumani.