Iran imeuza bidhaa katika nchi 142 duniani katika kipindi cha miezi saba
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i76692-iran_imeuza_bidhaa_katika_nchi_142_duniani_katika_kipindi_cha_miezi_saba
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanikiwa kuuza bidhaa zake katika nchi 142 katika kipindi cha miezi saba iliyopita.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 08, 2021 22:58 UTC
  • Iran imeuza bidhaa katika nchi 142 duniani katika kipindi cha miezi saba

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanikiwa kuuza bidhaa zake katika nchi 142 katika kipindi cha miezi saba iliyopita.

Hayo yamedokezwa na Ruhollah Latifi  msemaji wa Idara ya Forodha ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo amesema: "Tangu kuanza mwaka wa Hijria Shamsia (ulioanza Mach 21, 2021), Iran imefanikiwa kuuza nje ya nchi bidhaa za takribani tani milioni 99 zenye thamani ya takrbani dola bilioni 55.

Akifafanua kuhusu nchi ambazo zinanunua bidhaa kwa wingi kutoka Iran, Latifi amesema, "China, Iraq, Uturuki, Umoja wa Falme za Kiarabu na Afghansitan ndio nchi tano ambazo zimenunua bidhaa kwa wingi katika kipindi cha miezi saba iliyopita.

Aidha amesema moja ya sera ambazo zimekuwa zikifuatiliwa na Iran katika kipind cha miaka ya karibuni ni kuimarisha uuzaji nje bidhaa zisizo za mafuta ili kuimarisha sekta ya viwanda nchini.

Gari lililoundwa katika kiwanda cha Iran Khodro hapa nchini Iran

Biashara baina ya Iran na nchi jirani imekuwa ikiimarika katika miaka ya hivi karibuni. Iran ina mipaka na nchi 15 ambazo ni  Umoja wa Falme za Kiarabu, Afghanistan, Armenia, Jamhuri ya Azerbaijan, Bahrain, Iraq, Kuwait, Kazakhstan, Oman, Pakistan, Qatar, Russia, Uturuki Turkmenistan, na Saudi Arabia.

Pamoja na kuwepo vikwazo vya kidhalimu vya Marekani dhidi ya Iran, nchi nyingi duniani zina hamu kubwa ya kufanya biashara na Iran kutokana na uzalishaji wa bidhaa zenye viwango vya juu nchini.