Maonyesho ya Hijabu na Staha yafanyika Tehran
Maonyesho ya Bidhaa za Hijabu na Staha yamefunguliwa Tehran Jumatatu katika sherehe ambayo imehudhuriwa na gavana mpya wa Tehran Muhsin Mansuri.
Kwa mujibu wa taarifa maonyesho hayo yenye vibanda 300 yatafanyika kuanzia Novemba 2021 hadi Machi 2022 kwa lengo la kuunga mkono wafanya biashara wadogo wadogo na pia kuwahimiza wananchi kununia bidhaa hizo.
Akizungunza na mwandishi wa Iran Press wakati wa kufungua maonyesho hayo, Gavana wa Tehran amesema bidhaa zote zinazoonyeshwa katika maonyesho hayo zina sifa mbili mihimu nazo ni uzingatiwaji sifa za utamaduni na ustaarabu wa Kiislamu na Iran. Amesema wamejitahidi kuhakikisha kuwa bidhaa zote zilizo katika maonyesho hayo zinazingatia viwango vya Kiislamu na wakati huo huo umaridadi.
Muhsin Mansouri amesema maonyesho kama hayo yanaweza kufikiwa ile nara na kauli mbiu ya "Uzalishaji, Uwezeshaji na Uondoaji Vizuizi" sambamba na kuonyesha uwezo wa kitaifa.
Halikadhalika amesema maonyesho hayo yanaweza kuwa mfano wa kuigwa wa ushirikianno baina ya serikali na sekta binafsi.