Jan 02, 2022 04:26 UTC
  • Jihad al Islami: Kujitolea kikamilifu shahid Qasem Soleimani katika njia ya haki hakuwezi kusahaulika

Kiongozi mmoja mwandamizi wa ofisi ya kisiasa ya harakati ya Jihad al Islami ya Palestina amesema kuwa, kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qasem Soleimani na Abu Mahdi al Muhandis kumefungua njia kwa vijana wa eneo hili ya kupambana vilivyo na wanaoendesha njama za kulazimisha kukubalika utawala pandikizi wa Kizayuni.

Tovuti ya "Dunia al Watan" imemnukuu Bw. Yousuf al Hasayina  akisema hayo katika maadhimisho ya mwaka wa pili tangu alipouawa shahidi Luteni Jenerali Qasem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi (SEPAH) pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, aliyekuwa naibu wa mkuu wa vikosi vya kujitolea vya wananchi wa Iraq maarufu kwa jina la al Hashd al Shaabi na kusisitiza kuwa, kwa fadhila na baraka za Mwenyezi Mungu, kujitolea kikamilifu makamanda hao wa muqawama kumeleta mabadiliko makubwa na kuwasafishia njia vijana wa eneo hili ya kupambana vilivyo na njama za kuanzisha uhusiano wa kawaida na Wazayuni.

Luteni Jenerali Qasem Soleimani, aliyeuawa shahidi kwa kuipigania Quds, Kibla cha Kwanza cha Waislamu

 

Al Hasayina ameongeza kuwa, leo tunatanga tena utiifu wetu kwa malengo matakatifu ya Palestina na kuunga mkono taifa letu juhudi zote za kishujaa na za kujitolea muhanga mashahidi Soleimani na al Muhandis tukitangaza kwamba njia ya mashahidi wa Quds na Palestina kamwe haiwezi kusahaulika.

Kiongozi huyo mwandamizi wa harakati ya Jihad al Islami ya Palestina vile vile amesema, nguvu za kambi ya muqawama zinazidi kuwa kubwa siku baada ya siku na zinaleta matumaini ya kusambaratishwa utawala wa Kizayuni wa Israel na njama zote za mabeberu wa Magharibi na vibaraka wao katika eneo hili. 

Tags