Jan 07, 2022 13:19 UTC
  • Ayatullah Kazem Seddiqi
    Ayatullah Kazem Seddiqi

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema kuwa: Kambi iliyoasisiwa na shujaa Shahidi Qasem Soleimani katika vita vikali dhidi ya batili itawaangamiza kabisa Wamarekani na mamluki wao katika eneo hili la Magharibi mwa Asia.

Ayatullah Kazem Seddiqi amesema katika hotuba za Swala ya leo ya Ijumaa kwamba: "Shahid Qasem Soleimani aliwaunganisha pamoja kama minyororo mmoja watetezi wa Haram Tukufu kutoka Yemen, Lebanon, Afghanistan, Pakistan, Iraq, Iran na watu huru kote duniani kwa ajili ya kulinda matukufu na akabuni njia mpya ya mapambano.

Ayatullah Seddiqi ameongeza kuwa: “Licha ya mawazo ya rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump muuaji na mhalifu habithi na mahabithi wenzake, waliofanya jinai hiyo kwa amri yake wakidhani kwamba mapambano ya Jihadi yangedhoofika kwa kumuua kigaidi Shahidi Soleimani, Wamarekani hawatakuwa na utulivu hata siku moja katika eneo hili."

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran pia amesema: Wamarekani waliondoka Afghanistan kwa fedheha baada ya kuuawa shahidi Kamanda Soleimani.

Wamarekani wakiondoka kwa fedheha nchini Afghanistan

Ayatullah Seddiqi ameongeza kuwa: "Adui anayeonekana kuwa na nguvu katika masuala ya silaha, aliyeshindwa kisiasa, kijamii, kimaadili na kimataifa, alikumbana na pigo hilo kali na sasa haweza kufanya kosa lolote."

Vilevile ameashiria nafasi na sifa aali za Bibi Fatimatu Zahra (as), binti kipenzi wa Mtume wetu Muhammad (saw) aliyekufa shahidi siku kama ya jana tarehe 3 Jamadithani na kusema: Bibi Fatima alikusanya pamoja sifa zote njema na kuakisi kivitendo jamali na utukufu wa Mwenyezi Mungu SW. 

Tags