Jan 08, 2024 03:48 UTC

Kumbukumbu za kutimia mwaka wa nne tangu kuuliwa shahidi Luteni jenerali Shahidi Qassim Suleiman zimefanyika katika miji mikuu ya Nigeria na Ghana yaani huko Abuja na Accra kwa kuhudhuriwa na Waislamau wa matabaka mbalimbali na wafuasi wa kamanda huyo.

Luteni Jenerali Qassim Suleimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) waliuliwa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandes Naibu Mkuu wa Kikosi cha al Hashdu Shaabi cha Iraq na wanajihadi wenzake 8 Januari 3 mwaka 2020 katika shambulizi la anga lililotekelezwa na vikosi vamizi na kigaidi vya Marekani katika uwanja wa ndege wa Baghdad. 

Mashahidi, Kamanda Haj Qassim Suleimani na Abu Mahdi al Muhandes 

Shirika la habari la Iran Press limeripoti kuwa, wanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria wamemuenzi kamanda huyo shujaa wa Iran aliyeongoza  mapambano dhidi ya ugaidi kwa kushiriki huko Abuja katika hafla ya kutimia mwaka wa nne tanugu kuuliwa shahidi Kamanda Sueimani mwaka 2020.  

Shughuli hiyo ilifanyika chini ya nara "Kamanda Suleimani na Abu Mahdi al Muhandes"; Makamanda Wakubwa wa Ubinadamu" ambapo wazungumzaji walibainisha kuhusu shakhsia ya makamanda hao wawili wakuu wa mhimili wa muqawama.  

Katika marasimu hayo ya kumbukumbu ya mwaka wa nne tangu kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Qassim Suleimani,  Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Ghana pia amelaani mashambulizi ya kigaidi huko Kerman na kusema: Mauaji ya kizazi ya Wapalestina Ukanda wa Gaza yanatekelezwa na na utawala wa Kizayuni kwa kutumia silaha za Marekani. 

Hapa chini tumeweka baadhi ya picha za kumbukumbu hizo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Tags