Iran yawekea vikwazo Umoja wa Ulaya, Uingereza kwa kuchochea ghasia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i91630-iran_yawekea_vikwazo_umoja_wa_ulaya_uingereza_kwa_kuchochea_ghasia
Iran imewawekea vikwazo makumi ya maafisa na mashirika ya Umoja wa Ulaya (EU) na Uingereza kutokana na uungaji mkono wao na kuchochea ghasia mbaya za hivi karibuni nchini. Waliowekewa vikwazo wamekuwa wakitoa matamshi ya uingiliaji mambo ya ndani ya Jamhuri ya Kiislamu na pia wamekuwa wakiunga mkono ugaidi nchini Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 13, 2022 01:17 UTC
  • Iran yawekea vikwazo Umoja wa Ulaya, Uingereza kwa kuchochea ghasia

Iran imewawekea vikwazo makumi ya maafisa na mashirika ya Umoja wa Ulaya (EU) na Uingereza kutokana na uungaji mkono wao na kuchochea ghasia mbaya za hivi karibuni nchini. Waliowekewa vikwazo wamekuwa wakitoa matamshi ya uingiliaji mambo ya ndani ya Jamhuri ya Kiislamu na pia wamekuwa wakiunga mkono ugaidi nchini Iran.

Katika taarifa siku ya Jumatatu, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Nasser Kan'ani, alisema, "Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kufuatia vibali kutoka kwa mamlaka husika, ndani ya mfumo wa sheria na taratibu zinazohusiana na vikwazo na katika hatua ya kulipiza kisasi, inawekea vikwazo mashirika na taasisi kadhaa za Umoja wa Ulaya na Uingereza na hali kadhalika watu binafsi wa maeneo hayo kutokana na uungaji mkono wao wa makusudi kwa ugaidi na makundi ya kigaidi, na kuchochea kwao ugaidi, ghasia na chuki, ambayo imesababisha machafuko, vurugu, vitendo vya kigaidi na ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya taifa la Iran."

Machafuko yanayoungwa mkono na mataifa ya kigeni yamekumba maeneo mbalimbali ya Iran tangu mwanamke mwenye umri wa miaka 22 Mahsa Amini alipofariki katika hospitali Septemba 16, siku tatu baada ya kuanguka katika kituo cha polisi. Uchunguzi ulihusisha kifo cha Amini na hali yake ya kiafya ya huko nyuma, na si kupigwa na polisi kama ilivyodaiwa.

Hali baada ya hujuma ya kigaidi katika Haram ya Shah Cheragh nchini Iran

Machafuko yamepelekea kupoteza maisha makumi ya raia na maafisa wa usalama, huku pia yakipelekea kuibuka mashambulio ya kigaidi kote nchini. Katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, magaidi hao wanaopata himaya ya kigeni wamechoma moto mali ya umma na kuwatesa wanachama kadhaa wa Basij na vikosi vya usalama hadi kufa.

Tarehe 26 Oktoba, gaidi mwenye mafungamano na Daesh alishambulia Haram Takatifu ya Shah Cheragh katika mkoa wa kusini wa Fars kabla ya swala ya Magharibi na kuwauwa takribani waumini 15 akiwemo mwanamke na watoto wawili na kuwajeruhi wengine 40.

Takriban watu saba pia waliuawa baada ya magaidi kuwafyatulia risasi watu na vikosi vya usalama katika soko lililojaa watu katika jimbo la Khuzestan Izeh karibu na machweo ya Novemba 16.