Apr 06, 2023 03:34 UTC
  • Kiongozi wa Mapinduzi: Kimsingi hasa Wamagharibi ni maadui wa Haki za Binadamu

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Wamagharibi haiwaelekei kwa namna yoyote ile watoe madai ya haki za binadamu na akasisitiza kwamba, kimsingi hasa Wamagharibi ni maadui wa Haki za Binadamu.

Katika usiku wa kuadhimisha kuzaliwa Imam Hassan al Mujtaba AS hadhara ya malenga kadhaa wa lugha na fasihi ya Kifarsi na washairi vijana na wakongwe wa mashairi jana usiku walikutana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.

Katika mkutano huo, Ayatullah Khamenei alisisitiza kuwa Wamagharibi haiwaelekei kwa namna yoyote ile watoe madai ya haki za binadamu na akasisitiza kwamba, kimsingi hasa Wamagharibi ni maadui wa Haki za Binadamu na kila mtu alijionea haki zao za binadamu kwa DAESH (ISIS) za kuwachoma watu moto wakiwa hai au kuwagharikisha watu wakiwa hai, au katika kuwaunga mkono Munafikina (MKO) na Saddam au katika uhalifu dhidi ya Gaza na Palestina.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametaja uungaji mkono wa Wamagharibi kwa mauaji ya vijana waumini katika mitaa ya Tehran kuwa ni mfano mwingine wa madai ya uwongo ya kuunga mkono haki za binadamu na akaongezea kwa kusema: vijana wetu safi kabisa kimaadili kama  Arman Alivardi na Ruhollah Ajamian waliuawa kwa kuteswa na kwa uchochezi na mafunzo yaliyotolewa na vyombo vya habari vya Magharibi.

Mkutano wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na malenga na washairi

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Ayatullah Khamenei aliashiria hujuma za Magharibi dhidi ya Iran na akasema, kuweka vikwazo vya dawa na kuzuia utoaji wa chanjo kwa visingizio mbalimbali ni mifano mmojawapo wa hujuma za Wamagharibi dhidi ya Iran na akabainisha kwamba: lau kama wangeweza kufanya jambo la kuwawezesha kuinyima chakula pia Iran ya Kiislamu na watu wake, basi wasingesita kufanya hivyo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amegusia mfano mwingine wa anuai za hujuma za wanaoitakia mabaya Iran ambao ni wa hujuma za vyombo vya habari na kutumia kwao maelfu ya vyombo vya habari kueneza uwongo, uvumi na upotoshaji na akafafanua kwamba: "lengo la adui katika hujuma hizi ni kufuta nukta chanya za uwezo wa kifikra na kielimu na kudhoofisha moyo wa kujitegemea na kujitawala, istiqama ya kitaifa, umoja na kufanya mambo Kiislamu".

Ayatullah Khamenei amekutaja kudhoofisha kushikamana wanawake na dini kuwa ni nukta nyingine ya mawimbi ya hujuma zinazoelekezwa dhidi ya Iran na akaashiria nafasi na mchango athirifu na wenye taathira kubwa wa wanawake katika ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na hatua na marhala za baada yake na akaeleza kwamba: Wamagharibi hawamhurumii mwanamke wa Kiirani wala hawapiganii kuchungwa haki zake, bali wana chuki na uadui dhidi ya mwanamke wa Kiirani na wanajitangaza kiuwongo kwamba wanaunga mkono uhuru na haki za mwanamke wa Kiirani.../

Tags