-
Iran imetoa mikopo ya dola bilioni 28.7 kwa biashara, viwanda na familia katika kipindi cha miezi minne
Aug 14, 2024 11:26Takwimu za Benki Kuu ya Iran zinaonyesha kuwa kaya nchini zilipata asilimia 22.7 ya jumla ya mikopo iliyotolewa na mfumo wa benki nchini katika kipindi cha miezi minne hadi Julai 21.
-
Kiongozi Muadhamu atilia mkazo wajibu wa kusimama imara mbele ya vita vya kisaikolojia vya adui
Aug 14, 2024 09:00Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametilia mkazo wajibu wa kusimama imara kukabiliana na vita vya kisaikolojia vya adui akisema kuwa, wanaoendesha vita hivyo dhidi ya Iran wanajaribu kuzusha hofu na kulifanya taifa hili lilegeze kamba na lirudi nyuma katika nyuga tofauti.
-
Bagheri Kani: Uvamizi wa Wazayuni katika Msikiti wa Al-Aqsa unalenga kuzidisha mivutano
Aug 14, 2024 04:07Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema uvamizi wa baadhi ya mawaziri wa serikali ya utawala bandia wa Israel na walowezi wa Kizayuni katika msikiti wa al Aqsa ni hatua ya kichochezi inayolenga kushadidisha mivutano na ukosefu wa amani katika eneo.
-
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kwa mnasaba wa maadhimisho ya " Siku ya Muqawama wa Kiislamu"
Aug 14, 2024 03:52Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa taarifa na kupongeza kuadhimishwa "Siku ya Muqawama wa Kiislamu."
-
Iran: Hatuhitaji kibali kwa ajili ya kulinda usalama wa taifa na kumzuia adui
Aug 14, 2024 00:57Iran imesisitiza "haki yake inayotambuliwa" ya kutetea mamlaka ya kitaifa na kujenga kizuizi dhidi ya Israel kama chanzo cha ugaidi katika eneo hili, ikisema kuwa taifa hili halihitaji ruhusa kutoka kwa mtu yeyote" kuhusu suala hilo.
-
Kukanushwa tuhuma za Marekani dhidi ya Iran
Aug 13, 2024 22:52Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema, Marekani ndiyo muungaji mkono na muenezaji mkuu wa ugaidi katika eneo na dunia.
-
Sisitizo la China la kuunga mkono mamlaka ya kitaifa ya Iran
Aug 13, 2024 07:18Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa China Wang Yi anasema Beijing inaiunga mkono Iran katika kutetea "mamlaka yake, usalama na heshima ya taifa" huku Tehran ikiahidi kuiadhibu vikali Israel kutokana na mauaji ya aliyekuwa Ismail Haniyeh, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS.
-
Pezeshkian: Uungaji mkono wa Magharibi kwa Israel unahatarisha usalama wa kieneo na kiimataifa
Aug 13, 2024 07:16Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Irian amesema kuwa, kiimya cha jamii ya kimataifa mbele ya jinai dhidi ya binadamu zinazofanywa na utawala wa Kizayuni na ambazo hazijawahi kurekodiwa katika hiistoria, pamoja na uungaji mkono wa baadhi ya nchi za Magharibi kwa utawala huo dhalimu, ni mambo ambayo yanakwenda kinyume na sheia za kimataifa na yanachochea jinai zaidi kama ambavyo pia yanahatarisha usalama wa eneo hili na dunia nzima kwa ujumla.
-
Iran yatilia mkazo wajibu wa kukomeshwa haraka mauaji ya Ukanda wa Ghaza
Aug 13, 2024 07:15Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, Tehran sambamba na kuendelea na jitihada zake za kuhakikisha utawala wa Kizayuni unakomesha mashambulizi na ukatili wake huko Ghaza, inashikilia pia haki yake ya dhati na ya kisheria ya kuchukua hatua yoyote itakayoona inafaa kujibu jinai za Israel.
-
Iran: Marekani ndiye muungaji mkono na muenezaji mkuu wa ugaidi katika eneo na dunia
Aug 13, 2024 02:11Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema, Marekani ndiyo muungaji mkono na muenezaji mkuu wa ugaidi katika eneo na dunia.