-
Albanese: Israel ifukuzwe UN kwa kubomoa makao makuu ya UNRWA
Jan 24, 2026 07:03Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu ameilaani Israel kwa kubomoa makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina (UNRWA) katika mji wa Baitul Muqaddas Mashariki unaokaliwa kwa mabavu, na kutaka kusimamishiwa unachama utawala huo wa Kizayuni katika Umoja wa Mataifa.
-
Kamanda: Iran itatoa majibu makali kwa vitisho vya Trump
Jan 24, 2026 04:27Kamanda mwandamizi wa jeshi la Iran amesema kwamba Jamhuri ya Kiislamu iko tayari na ina hakika itajibu kwa nguvu vitisho na kauli za Rais wa Marekani, Donald Trump.
-
Ripoti: Netanyahu hakuenda Davos kutokana na hofu ya kukamatwa
Jan 24, 2026 04:26Vyombo vya habari vya utawala wa Israel vimeripoti kwamba Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, hakuhudhuria Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) mjini Davos wiki hii kutokana na wasiwasi kwamba angeweza kukamatwa nchini Uswisi kufuatia hati ya kukamatwa iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
-
Iran yalaani kikao cha UNHRC, yasema haitasalimu amri mbele ya mashinikizo ya kigeni
Jan 24, 2026 04:25Iran siku ya Ijumaa ilipinga kikao maalum cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC), ikikitaja kuwa hakina uhalali. Mjumbe wa Iran mjini Geneva alisisitiza kwamba Iran halijawahi na halitakubali kutawaliwa au kushinikizwa na nguvu za kigeni.
-
Uchunguzi wa maoni waonyesha wengi Ulaya wanamwona Trump kama ‘adui’ kuliko ‘rafiki
Jan 24, 2026 04:25Uchunguzi mpya wa maoni umebaini kwamba katika baadhi ya nchi kubwa barani Ulaya, watu wengi zaidi wanamwona rais wa Marekani kama “adui” kuliko “rafiki” au mshirika wa Ulaya.
-
Serikali ya Msumbiji yaomba msaada wa haraka wa kimataifa kufuatia mafuriko makubwa
Jan 24, 2026 04:24Serikali ya Msumbiji imeomba Ijumaa kwamba jumuiya ya kimataifa ichukue hatua za dharura za kibinadamu ili kukabiliana na mafuriko makubwa ambayo yamesababisha maelfu kwa maelfu kuyahama makazi yao na kuharibu miundombinu katika taifa hilo la Kusini Mashariki mwa Afrika.
-
Iran yamjibu Zelensky; yamwambia dunia imechoka na 'vikaragosi vilivyochanganyikiwa'
Jan 24, 2026 00:02Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi amemkosoa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky kwa kuingilia masuala ya ndani ya Jamhuri ya Kiislamu, na kumwambia bayana kwamba dunia imechoka na "Wanaserere Waliochanganyikiwa."
-
Hizbullah: Vitisho vya US dhidi ya Kiongozi Muadhamu vitateketeza eneo lote
Jan 24, 2026 00:01Tawi la Kisiasa la Harakati ya Muqawama ya Hizbullah katika Bunge la Lebanon limeonya kwamba, vitisho vya maneno vya Marekani dhidi ya Iran na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei vinaweza kushadidisha mvutano katika eneo la Asia Magharibi.
-
Starmer amtaka Trump aombe radhi kwa kauli ya 'kutusi' aliyotoa kuhusu uvamizi wa Afghanistan
Jan 24, 2026 00:01Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer ametaka Rais wa Marekani Donald Trump aombe radhi kwa madai yake kwamba wanajeshi wa Ulaya hawakuwa mstari wa mbele katika vita vya kivamizi vya mwaka 2001 vilivyoanzishwa na Marekani na waitifaki wake dhidi ya Afghanistan.
-
DA yakanusha madai ya Trump ya kuwepo mauaji ya Wazungu A/Kusini
Jan 23, 2026 23:18Kiongozi wa chama cha Democratic Alliance cha Afrika Kusini (DA), John Steenhuisen amekadhibisha madai ya kuwepo "mauaji ya kimbari ya Wazungu" nchini Afrika Kusini.