-
Israel yakiri: Iran ilikuwa na uwezo wa kumlenga kwa hujuma za mtandao kila Muisraeli katika Vita vya Siku 12
Dec 11, 2025 03:42Mkuu wa idara ya usalama wa kimtandao ya utawala wa kizayuni wa Israel (INCD) amesema, operesheni za kimtandao za Iran za wakati wa vita vya siku 12 mnamo mwezi Juni zilikuwa na wigo mpana kutosha kumfikia kila raia wa Israel na kwamba Tehran ilikuwa ikipanga na kufanya mashambulizi ya makombora dhidi ya maeneo yaliyolengwa kama vile Taasisi ya Weizmann kwa kudukua kwanza kamera za usalama za maeneo hayo.
-
Tangu ulipotangazwa usitishaji vita Ghaza, Israel imewaua shahidi Wapalestina wasiopugua 386
Dec 11, 2025 03:42Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Habari ya Ukanda wa Ghaza ametangaza kuwa jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel halijaheshimu wala kufungamana na makubaliano ya kusitisha mapigano na itifaki ya masuala ya kibinadamu iliyoainishwa kwenye makubaliano hayo.
-
Watu 22 wafariki, 16 wajeruhiwa baada ya majengo mawili kuporomoka katika mji wa Fes, Morocco
Dec 11, 2025 02:41Watu wapatao 22 wamefariki dunia na wengine 16 wamejeruhiwa wakati majengo mawili ya makazi ya watu yalipoporomoka katika mji wa Fes ulioko kaskazini mwa Morocco, jana Jumatano.
-
Kwa kuhofia Trump asije akafuatiliwa, White House yatoa vitisho, yaitaka ICC iifanyie mabadiliko hati yake
Dec 11, 2025 02:40Shirika la habari la Reuters limezinukuu duru za kuaminika na kuripoti kuwa, serikali ya Marekani imewasiliana kwa siri na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC na kutishia kuiwekea vikwazo vipya ikiwa itajaribu kumshtaki Rais wa Marekani Donald Trump kwa uwezekano wa kuhusika na uhalifu.
-
Ghana yajibu mapigo kwa Israel, yawatimua wazayuni watatu waliowasili nchini humo
Dec 11, 2025 02:40Serikali ya Ghana imewatimua kwa kuwarejesha walikotoka Waisraeli watatu, katika hatua ya kujibu mapigo na kulipiza kisasi dhidi ya utawala wa kizayuni wa Israel baada ya hapo awali kulalamikia kunyanywaswa raia wake katika uwanja wa ndege wa Ben Gurion, mjini Tel Aviv.
-
Ansarullah: Wazayuni wawafanyia ukatili hata wanawake wajawazito
Dec 11, 2025 00:06Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen, ametoa hotuba kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake na kugusia jinsi utawala wa Kizayuni wa Israel unavyoua kikatili maelfu ya wanawake Waislamu nchini Palestina wakiwemo wanawake wajawazito, wazee na watoto na kusema kuwa, Wazayuni hawawaonei huruma hata wanawake wajawazito na vitoto vichanga vilivyomo tumboni.
-
Pezeshkian: Hatua ya Marekani dhidi ya Venezuela ni uzushi hatari unaotishia amani ya dunia
Dec 11, 2025 00:05Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amekosoa na kulaani waziwazi vitendo haramu vya Marekani katika eneo la Karibi, akisema: "Kitendo cha serikali ya Marekani cha kutuma meli za kivita huko Karibi na pwani ya Venezuela, kwa visingizio vya uwongo, ni haramu, ukiukaji wa sheria za kimataifa na ni uzushi hatari unaotishia amani na usalama wa dunia."
-
Ghana yakosoa vitendo vya kinyama vya Israel dhidi ya raia wa nchi hiyo waliokwenda mkutanoni Tel Aviv
Dec 11, 2025 00:05Ghana jana Jumatano kile ilikosoa kile ilichokitaja kuwa vitendo vya "kinyama" walivyotendewa raia wa nchi hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) baada ya wasafiri kadhaa wa Ghana kuzuiliwa au kufukuzwa .
-
Ripoti: Asilimia 10 ya watu duniani wanamiliki asilimia 75 ya utajiri wa dunia
Dec 11, 2025 00:03Ripoti iliyotolewa na The Global Economic Inequality (GEI) kuhusu ukosefu wa usawa wa kiuchumi duniani imeonya pengo linaloongezeka kati ya matajiri na maskini na haja ya dharura la kushughulikia mgogoro huu, ikisema: asilimia 10 ya idadi ya watu duniani wanamiliki asilimia 75 ya utajiri wote wa dunia.
-
Rwanda yayatuhumu majeshi ya Kongo na Burundi kwa kukiuka makubaliano ya amani ya Washington
Dec 11, 2025 00:02Rwanda imeyatuhumu majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burundi kuwa yamekiuka usitishaji mapigano kwa mujibu wa makubaliano ya amani yaliyofikiwa karibuni huko Washington kwa lengo la kuhitimisha hali ya mchafukoge mashariki mwa Kongo.