-
Mapigano kati ya jeshi la Ethiopia na Tigray yapanuka hadi mpakani mwa Sudan
Aug 04, 2026 10:22Makabiliano ya kijeshi kati ya vikosi vya Serikali ya Shirikisho nchini Ethiopia na Kikosi cha Ukombozi wa Watu wa Tigray yanaongezeka baada ya siku kadhaa za mapigano, na sasa yanaripotiwa kupanuka hadi kwenye maeneo ya mpakani na Sudan.
-
Algeria na Italia zakubaliana kuimarisha ushirikiano ili kupambana na uhamiaji haramu
Aug 04, 2026 10:19Algeria na Italia zimekubaliana kuimarisha ushirikiano dhidi ya uhamiaji haramu na uhalifu wa kuvuka mipaka. Uamuzi huu umefikiwa wakati wa mazungumzo kati ya Mawaziri wa Mambo ya Ndani wan chi mbili hizo huko Roma, Italia.
-
Leo ni Arubaini ya Imam Hussein AS, Waislamu wa Iran waungana na Waislamu wengine kuiadhimisha
Aug 04, 2026 03:14Jumanne ya leo ya tarehe 4 Agosti 2026 inasadifiana na maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussein AS, yaani siku ya 40 tangu Imam Husain AS na wafuasi wake watiifu walipouawa kinyama kwenye jangwa la Karbala mwezi 10 Mfunguo Nne Muharram, mwaka wa 61 Hijria.
-
Baghaei: Mashambulizi ya Marekani dhidi ya maeneo ya raia nchini Iran ni uhalifu wa kivita
Aug 04, 2026 03:09Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, amesema mashambulizi ya Marekani dhidi ya maeneo ya makazi na ya raia katika miji ya Qeshm, Minab, na Lamerd ni uhalifu wa kivita, huku akiahidi kuwa Iran itatumia mifumo yote ya kimataifa inayopatikana kuwafikisha wahalifu mbele ya sheria.
-
Jeshi la Iran laangusha ndege ya kivita ya Marekani ya MQ-9 Reaper katika Lango la Hormuz
Aug 04, 2026 03:08Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza rasmi kuwa kikosi chake cha anga kimeidungua ndege ya kivita isiyo na rubani ya Marekani aina ya MQ-9 Reaper juu ya Lango la Hormuz, kwa kutumia mfumo wa ulinzi wa anga ulio wa kisasa na wenye uwezo wa hali ya juu.
-
Afisa wa Ansarullah: Kauli za Trump kuhusu amani zimetokana na hofu ya nguvu za Iran
Aug 04, 2026 03:04Afisa mwandamizi wa Ansarullah amesema kuwa matamshi ya hivi karibuni ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu amani yanaonyesha wasiwasi wa Marekani juu ya uwezo wa ulinzi wa Iran.
-
WHO: DRC inakabiliwa na mlipuko mbaya zaidi wa Ebola katika historia
Aug 04, 2026 03:02Shirika la Afya Duniani (WHO) limetahadharisha kuwa mlipuko wa Ebola unaoendelea kusambaa kwa kasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ndio mkubwa zaidi kuwahi kuikumba nchi hiyo katika rekodi zake zote.
-
Baqaei: Hakuna mazungumzo na Washington kwa sasa, tunajadiliana na Oman kuhusu njia ya muda Lango-Bahari la Hormuz
Aug 03, 2026 11:14Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: "Hatufanyi mazungumzo na Marekani, na mazungumzo yetu na Oman yanahusu njia ya kupita salama meli katika Lango-Bahari la Hormuz."
-
Rais wa Somalia: Tutazuia Israel kuimarisha ushawishi wake Somaliland
Aug 03, 2026 11:10Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, amesema kwamba Serikali ya Shirikisho itachanganya "nguvu na hekima" ili kuzuia "Israel" kupata nafasi au kuanzisha ushawishi wa kudumu katika eneo la "Somaliland," akisisitiza kwamba Mogadishu ingali inashikamana na umoja wa ardhi na mamlaka ya Somalia, na inapinga kwa nguvu zote kuhamisha migogoro ya "Mashariki ya Kati" hadi eneo la Pembe ya Afrika.
-
Kwa nini shambulio la Saudi Arabia na Marekani dhidi ya Hashd al-Shaabi ni ukiukaji wa wazi wa mamlaka ya kujitawala ya Iraq?
Aug 03, 2026 11:09Kikosi cha Hashd al-Shaabi cha Iraq kilitangaza siku chache zilizopita kuwa watu wasiopungua 20 waliuawa na wengine 32 kujeruhiwa katika shambulio la pamoja la kichokozi lililofanywa na Marekani na Saudi Arabia dhidi ya Iraq mapema Jumatano iliyopita.