Leon Panetta: Vita dhidi ya Iran imekuwa Vietnam nyingine kwa Trump
-
Leon Panetta
Waziri wa zamani wa Vita wa Marekani ameonya kuwa: Vita dhidi ya Iran vinakuwa sawa na vita Vietnam kwa Rais wa Marekani, Donald Trump.
Leon Panetta ameiambia CNN kwamba: "Vita dhidi ya Iran inazidi kuwa kama Vietnam kwa Trump. Tulifanya mazungumzo huko Vietnam, lakini mwishowe, Vietnam Kaskazini ilichukua udhibiti kamili." Amesema Panetta na kuongeza kuwa: "Haijalishi ni makubaliano gani tutakayofanya na utawala wa Iran wenye msimamo thabiti, watadhibiti Mlango-Bahari wa Hormuz na watafanya lolote wawezalo kuendeleza urutubishaji wa urani."
Afisa huyo wa zamani wa Marekani amesisitiza kuwa: "Kwa kuzingatia uhakikisho ulilokuwa amepewa na Israel, Trump alidhani kwamba utawala wa Iran ungesambaratika ndani ya siku chache mara tu viongozi wake watakapouawa. Yalikuwa mahesabu mabaya sana."
Wakati huo huo, vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kuwa soko la hisa la nchi hiyo limepitia siku yake mbaya zaidi tangu Oktoba mwaka jana. Ripoti zinasema uuzaji mkubwa wa hisa za makampuni makubwa ya teknolojia umeweka mashinikizo makubwa kwenye soko kwa ujumla.