-
Baada ya Israel kuwaua Wapalestina wengine 24 Ghaza, HAMAS yataka wapatanishi, hasa US iingilie kati
Nov 23, 2025 03:35Jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel limefanya mashambulizi makali ya anga katika maeneo tofauti ya Ukanda wa Ghaza, na kuwaua shahidi Wapalestina wasiopungua 24, wakiwemo watoto, katika mwendelezo wa ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa tangu wiki sita zilizopita kwenye eneo hilo la Palestina lililoteketezwa kwa vita.
-
Marekani yabatilisha viza ya waziri wa zamani wa Afrika Kusini aliyefanikisha kesi ya ICJ dhidi ya Israel
Nov 23, 2025 03:31Marekani imefuta viza ya waziri wa zamani wa Mahusiano ya Kimataifa wa Afrika Kusini Naledi Pandor mapema wiki hii, katika kile kinachoonekana kama hatua za hivi karibuni za Washington za kuiadhibu Pretoria kwa sababu kuuburuza utawala wa kizayuni wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kwa mauaji ya kimbari uliyofanya dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.
-
Wanafunzi 303, walimu 12 watekwa nyara na watu wenye silaha katika skuli ya jimbo la Niger, Nigeria
Nov 23, 2025 03:03Jumuiya ya Wakristo ya Nigeria (CAN) imetangaza kuwa, jumla ya wanafunzi 303 na walimu 12 wametekwa nyara na watu wenye silaha wasiojulikana likiwa ni tukio la pili kubwa kutokea ndani ya wiki moja, huku hofu za usalama zikiongezeka katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika.
-
Rais Macron wa Ufaransa atoa indhari: G20 inakaribia kusambaratika
Nov 23, 2025 03:03Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, ameeleza katika hotuba isiyo ya kawaida aliyotoa katika mkutano wa nchi zinazounda G20 mjini Johannesburg, Afrika Kusini kwamba kundi hilo limepoteza uwezo wake wa kuwa na taathira ya kutatua migogoro ya kimataifa na kwamba linakaribia kusambaratika.
-
Katika mkutano na Trump, Mamdani azungumzia US inavyofadhili mauaji ya kimbari Ghaza
Nov 23, 2025 03:02Zohran Mamdani, Meya mpya mteule wa Jiji la New York, amezungumzia suala la ufadhili wa Marekani kwa vita vya mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza, katika mkutano aliofanya na rais wa Marekani Donald Trump Ikulu ya White House.
-
Kamanda: Jeshi la Iran liko tayari kukabiliana na tishio lolote
Nov 22, 2025 23:42Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu la Iran, akizungumza mbele ya makamanda wenzake, amesisitiza kuwa kwa kuzingatia maelekezo ya Kiongozi Muadhamu na kwa kutumia tajiriba ya vita vya zamani, hususan vita vya kulazimishwa vya siku 12 vya mwezi Juni, jeshi limeweka mkakati wa kuzingatia nguzo tano: utii wa uongozi, uadilifu, ufanisi, teknolojia na uboreshaji wa ujuzi.
-
Uozo ndani ya jamii ya Israel, wanawake 3,000 wadhalilishwa kijinsia jeshini
Nov 22, 2025 23:38Jumuiya ya Vituo vya Mgogoro wa Ubakaji ndani ya utawala wa Kizayuni imefichua katika ripoti yake ya kila mwaka kuweko ongezeko kubwa la ukatili wa kijinsia na jinsi serikali ya utawala huo inavyochuja mno na kufanya usiri mkubwa wa ukatili huo ndani ya taasisi zake za kiusalama.
-
Mkutano wa viongozi wa G20 wafunguliwa Afrika Kusini kwa hotuba ya Rais Ramaphosa
Nov 22, 2025 23:37Mkutano wa viongozi wa G20 umefunguliwa Jumamosi mjini Johannesburg, Afrika Kusini, ambapo Rais Cyril Ramaphosa alitoa hotuba ya kwanza wakati wajumbe walipokusanyika kwa mazungumzo ya siku mbili.
-
Madini ya risasi na zinki yaimarisha hadhi ya Iran kama ngome ya madini Asia Magharibi
Nov 22, 2025 23:37Tarehe 22 Novemba, huadhimishwa kitaifa nchini Iran kama Siku ya Madini ya Risasi na Zinki ikiwa ni kuashiria nafasi kuu ya sekta hii na uhusiano wake wa karibu na malengo ya kiuchumi ya taifa.
-
Jeshi la Sudan linasonga mbele Kordofan katika mapambano na waasi wa RSF
Nov 22, 2025 23:36Jeshi la Sudan limeendelea kusonga mbele katika maeneo ya Kordofan Kaskazini na Kordofan Magharibi mwishoni mwa wiki, kufuatia mapigano makali na waasi wa Rapid Support Forces (RSF), kwa mujibu wa vyanzo vya kijeshi.