-
Reuters: Serikali ya Trump inafikiria kuizuia Saudia ndege za kisasa za kivita za F-35
Nov 05, 2025 23:49Shirika la habari la Reuters limenukuu chanzo cha kuaminika ambacho hakikutaka kitajwe na kutangaza kwamba serikali ya Trump inapitia ombi la Saudi Arabia la kununua ndege 48 za kivita za kisasa za F-35, mpango wa mabilioni ya dola ambao umeondoa moja ya vikwazo vikubwa katika Wizara ya Vita ya Marekani na ambao unajadiliwa sanjari na ziara ijayo ya Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman huko nchini Marekani.
-
Mahakama ya Juu Mauritania yaidhinisha kifungo cha miaka 15 jela alichohukumiwa rais wa zamani
Nov 05, 2025 22:59Rais wa zamani wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz, ameshindwa katika rufaa yake ya mwisho aliyokata ya kupinga kifungo cha miaka 15 jela alichohukumiwa baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na ufisadi alipokuwa madarakani. Mahakama ya Juu ya Mauritania imeidhinisha hukumu hiyo.
-
Zaidi ya Wapalestina 9,000 wanashikiliwa katika jela za Israel
Nov 05, 2025 15:33Taasisi tatu za Palestina zinazohusiana na masuala ya mateka zimetangaza kuwa, utawala wa Israel unawashikilia Wapalestina 9,250 katika jela zake.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Tuzo ya Nobel imepoteza itibari kwa mpokeaji kumsifu Netanyahu
Nov 05, 2025 09:10Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amekosoa tuzo ya Nobel ya Amani ya mwaka 2025, na kusema tuzo hiyo imepoteza uhalali wake kutokana na kupewa kwa Maria Corina Machado, ambaye amemsifu Benjamin Netanyahu licha ya kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita.
-
Iran yataka UN ichukue hatua kufuatia kauli ya Trump kuhusu majaribio ya silaha za nyuklia
Nov 05, 2025 09:08Iran imetoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukutana kwa dharura kufuatia kauli za “kushtua sana” zilizotolewa na Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu kuanza tena majaribio ya silaha za nyuklia.
-
Nigeria yapinga madai ya Trump kuhusu mauaji ya Wakristo
Nov 05, 2025 09:07Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria, Yusuf Tuggar, amepinga madai ya Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu mauaji ya Wakristo nchini Nigeria, akionya dhidi ya kauli zinazoweza kuchochea mgawanyiko wa kidini au kikabila nchini humo.
-
Maonesho ya 16 ya Teknolojia ya Nano ya Iran yafanyika Tehran
Nov 05, 2025 09:06Maonesho ya 16 ya Teknolojia ya Nano ya Iran yamefanyika katika Uwanja wa Maonesho wa Kimataifa jijini Tehran, yakileta pamoja zaidi ya kampuni 150 za kiteknolojia.
-
Kamanda wa RSF ajigamba kuwaua raia 2,000 El Fasher, Sudan; ICC yaanza uchunguzi
Nov 05, 2025 09:05Video za kushtua zimeibuka zikimuonesha kamanda wa kikundi cha waasi wa RSF nchini Sudan akijigamba kwa kuwaua binafsi zaidi ya raia 2,000 wakati wa utekaji wa mji wa El Fasher ulioko Darfur.
-
Sudan: Jamii ya kimataifa ichukue hatua kusitisha utumaji silaha kwa wanamgambo wa RSF
Nov 05, 2025 03:42Sudan imekariri wito wake kwa jamii ya kimataifa ikitaka kufanyika juhudi za kuzuia mtiririko wa silaha kwa wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) na kulitaja kundi hilo kuwa "taasisi ya kigaidi."
-
UN: Askari usalama wa Cameroon wauwa raia 48 katika maandamano ya kupinga uchaguzi wa rais
Nov 05, 2025 03:41Duru za Umoja wa Mataifa zimeripoti kuwa askari usalama wa Cameroon wameuwa raia 48 katika maandamano ya kupinga kuchaguliwa tena Rais Paul Biya, mtawala mzee zaidi duniani.