-
Qalibaf: Vita vya siku 12 vimethibitisha kuwa 'uadui' wa Marekani dhidi ya Iran 'unaendelea'
Nov 04, 2025 09:18Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, ametangaza kwamba vita vya hivi karibuni vya siku 12 vimefichua uadui unaoendelea wa Marekani, akisisitiza kwamba ingawa mbinu zake zimebadilika, lakini lengo lake la msingi la kupinga Iran yenye nguvu na huru bado halijabadilika.
-
Tehran yasema 'vita halisi vya kikanda' na Israel vinaendelea, yapuuza mazungumzo na Marekani
Nov 04, 2025 08:07Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran amesema kwamba eneo la Magharibi mwa Asia kwa sasa limo katika na "vita halisi" na utawala wa Israel, akisisitiza kwamba hali ya eneo hilo iimekwenda mbali zaidi ya vitisho tu.
-
Nyaraka za jeshi la Israel zafichua: Mfungwa wa Kipalestina aliyebakwa alikuwa raia, si mpiganaji
Nov 04, 2025 07:48Waraka wa siri wa jeshi la Israel umefichua kwamba mtu aliyeshambuliwa kikatili na kubakwa na kundi la wanajeshi wa Israel katika gereza maarufu la Sde Teiman mnamo Julai mwaka jana hajawahi kushtakiwa kwa uhalifu wowote na alikuwa raia, kinyume na madai kwamba alikuwa na mwanachama harakati za mapambano ya Hamas.
-
Guterres: Uhalifu wa kivita nchini Sudan hauwezi kupita hivihivi bila kuadhibiwa
Nov 04, 2025 07:47Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka ili kusimamisha mapigano nchini Sudan, akisisitiza kwamba moja ya masharti muhimu ya kukomesha vita ni kuzuia silaha mpya kuingia nchini humo, na kusisitiza kwamba kuendelea mtiririko wa silaha kunarefusha mzozo na kuzidisha mateso ya raia.
-
Tarehe 13 Aban; dhihiriisho la mshikamano wa kitaifa kwa ajili ya kukabiliana na sera za uingiliaji kati za Marekani nchini Iran
Nov 04, 2025 07:02Tarehe 13 Aban (4 Novemba) inafahamika katika kalenda ya Iran kama "Siku ya Taifa ya Kupambana na Uistikbari Duniani".
-
Israel inatumia wanasesere waliotegwa mabomu kuua watoto wachanga huko Gaza
Nov 04, 2025 06:50Wizara ya Afya ya Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umetega mabomu kwenye wanasesere ili kuwaua watoto wa Palestina.
-
Maandamano ya Siku ya Kupambana na Ubeberu yanaendelea hivi sasa kwenye miji 900 ya Iran
Nov 04, 2025 03:31Maandamano ya Siku ya Mwenyezi Mwenyezi Mungu yaani Aban 13 ambayo ni Siku ya Taifa ya Iran ya Kupambana na ubeberu na uistikbari yanaendelea hivi sasa hapa mjini Tehran na katika zaidi ya miji 900 kote humu nchini.
-
Duru za Israel: Hizbullah imeshajijenga upya, sasa tusubiri vita
Nov 04, 2025 03:30Mashirika ya usalama ya Israel yametangaza kwamba yanajiandaa kwa ajili ya kuingia kwenye vita vikubwa na Hizbullah ya Lebanon yakidai kuwa harakati hiyo imeshajijenga upya kijeshi na sasa lazima wasubiri majibu makali kutoka kwa harakati hiyo.
-
Majasusi watano wa Israel watiwa mbaroni Ghaza
Nov 04, 2025 03:30Kikosi cha kujihami kiitwacho "Rad'e" kinachoshirikiana na Muqawama kwa ajili ya kulinda usalama huko Ghaza, jana Jumatatu kilifanya operesheni ya kiusalama kusini mwa mji wa Khan Yunis na kuwatia mbaroni majasusi watano wa Israel.
-
Waziri al Sudani: Wananchi wataendelea kubeba silaha madamu Marekani bado ipo Iraq
Nov 04, 2025 03:28Waziri Mkuu wa Iraq, Mohammed al-Sudani alisema jana Jumatatu kwamba kuondoka kikamilifu Marekani na muungano wake unaodaiwa wa kupambana na Daesh huko Iraq ndiko kutakakopelekea kupokonywa silaha makundi ya kujihami ya wananchi. Kwa mujibu wa makubaliano, Marekani lazima iondoke Iraq mwezi Septemba mwaka ujao wa 2026.