-
Israel yashambulia kusini mwa Lebanon; raia mmoja auawa
Oct 30, 2025 08:54Wanajeshi wa Israel wamefanya shambulizi la nchi kavu katika mkoa wa kusini mwa Lebanon wa Nabatieh, huo ukiwa ukiukaji mwingine wa makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yalianza kutekelezwa karibu mwaka mmoja uliopita.
-
Vyombo vya habari vinavyotumikia jinai (Google; mshirika katika jinai za Netanyahu)
Oct 30, 2025 08:51Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni katika kipindi chetu cha Makala ya Wiki. Kipindi hiki kinachunguza dhulma ya vyombo vya habari kuanzia namna taarifa zilivyokusanywa na kufikishwa kwa watu hadi matangazo kuhusu kampeni za kipropaganda zilizofanywa na serikali ya Israel na kinafafanua ni kwa namna gani ueledi wa masuala ya vyombo vya habari na haja ya kuwepo uwazi vinaweza kudhihirisha uhakika na kuutoa chini ya vifusi vya upotoshaji. ******
-
Iran: Mkuu wa IAEA anapasa kuepuka ‘matamshi yasiyo na msingi’ kuhusu miradi ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya kiraia
Oct 30, 2025 08:51Iran imesema kuwa Rafael Grossi Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) anajia “kikamilifu” namana miradi ya nishati ya nyuklia ya nchi hii ilivyo ya malengo ya amani na ya kiraia; kwa hiyo anapasa kujiepusha kutoa “matamshi yasiyo na msingi” kuhudu miradi hiyo.
-
Trump aiamuru Wizara ya Vita ya Marekani kuanza tena majaribio ya silaha za nyuklia
Oct 30, 2025 08:47Rais Donald Trump wa Marekani ameiagiza Wizara ya Vita ya nchi hiyo kuanza tena majaribio ya silaha za nyuklia; katika uamuzi ambao umewatia wasiwasi wapinzani wa silaha za maangamizi ya umati na wataalamu masuala ya usalama duniani.
-
Belarus yadhamiria kukuza uhusiano na Iran
Oct 30, 2025 08:34Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus, Maxim Ryzhenkov, amesema nchi yake imedhamiria kukuza uhusiano na Iran katika nyanja mbalimbali.
-
Agizo la Trump la kuanza tena majaribio ya silaha za nyuklia; Dunia inarudi kwenye mashindano ya silaha za nyuklia?
Oct 30, 2025 08:22Rais Donald Trump wa Marekani ameamuru kuanzishwa tena majaribio ya silaha za nyuklia za nchi hiyo.
-
Grossi: Hakujaonekana ongezeko la urutubishaji urani nchini Iran
Oct 30, 2025 03:17Licha ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA kutangaza kuwa hakuna ongezeko lolote la urutubishaji urani nchini Iran, lakini wakati huo huo amedai kuwa kumeonaka harakati mpya katika vituo vya nyuklia vya Iran.
-
Marekani kuunda kikosi kipya cha kijeshi cha kukandamiza raia
Oct 30, 2025 03:17Wizara ya Vita ya Marekani imeamuru wanajeshi wa Gadi ya Taifa kuunda kikosi kipya haraka kwa ajili ya kukandamiza zaidi raia wanaolalamikia uongozi mbovu wa Trump katika majimbo yote ya Marekani. Kikosi hicho kitapewa nguvu zote za kukandamiza maandamano ya wananchi ya kupigania haki zao.
-
Miili 460 ya watu yapatikana hospitalini El Fasher, mawaziri wa Sudan na Misri wakutana
Oct 30, 2025 03:16Zaidi ya wagonjwa 460 na watu walioandamana nao wameripotiwa kupatikana wameuawa katika hospitali ya uzazi huku kukiwa na ripoti za kuendelea ukatili dhidi ya raia huko El Fasher, Sudan. Hayo yameripotiwa huku mawaziri wa Mambo ya Nje wa Sudan na Misri wakikutana kujadiliana hali ya eneo hilo la magharibi mwa Sudan.
-
Angola yatangaza kuwekeza kwenye satelaiti mpya
Oct 30, 2025 03:16Serikali ya Angola imetangaza kuwa itaongeza uwekezaji katika sekta ya mawasiliano ya simu, ambao utajumuisha mpango wa kurusha satelaiti mpya ya uchunguzi na kupanua mtandao wa taifa wa mawasiliano kama sehemu ya mkakati mpana wa kufaidika vizuri na teknolojia za kisasa zinazojumuisha watu wote nchini humo.