-
Jeshi la Sudan lapambana na waasi wa RSF katika miji ya el-Fasher na Bara
Oct 26, 2025 04:35Mapigano yamezidi kushadidi maeneo kadhaa ya Sudan baada ya waasi wa RSF kuendeleza mashambulizi dhidi ya mji wa el-Fasher ulioko Kaskazini mwa Darfur, pamoja na mji wa Bara katika mkoa wa Kordofan Kaskazini.
-
Araghchi: Iran iko tayari kwa mazungumzo ya kidiplomasia na Marekani kwa msingi wa kuheshimiana
Oct 26, 2025 04:35Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema kuwa Tehran iko tayari kushiriki katika mazungumzo ya kidiplomasia na Marekani ili kufikia “suluhisho la busara” kuhusu suala la nyuklia, kwa misingi ya usawa na kuheshimiana pande zote.
-
Muungaji mkono Palestina achaguliwa kuwa rais wa Ireland
Oct 26, 2025 04:34Bi. Catherine Connolly, mgombea wa mrengo wa kushoto katika uchaguzi wa urais nchini Ireland ambaye anajulikana kwa misimamo yake ya kuunga mkono Palestina, ameibuka mshindi katika uchaguzi huo.
-
Ethiopia na Somalia zaahidi amani katika eneo wakati wa Jukwaa la 11 la Tana
Oct 26, 2025 04:33Ethiopia na Somalia zimeithibitishia dunia dhamira yao ya kudumisha amani ya kikanda wakati wa Jukwaa la 11 la Tana ambalo limejadili jukumu la kimkakati la Pembe ya Afrika.
-
Malaysia yashuhudia maandamano makubwa dhidi ya Israel na Marekani
Oct 26, 2025 02:39Maandamano makubwa yamefanyika nchini Malaysia kuunga mkono wananchi wa Palestina na kulaani himaya ya Marekani kwa Israel na jinai za utawala huo ghasibu katika Ukanda wa Gaza.
-
Kwa nini UNRWA huko Gaza inalengwa kwa mashinikizo ya kisiasa?
Oct 26, 2025 02:39Mkuu wa Shirika la Misaada na Ajira kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) amesema: Vita vya Gaza vimeonyesha kwamba sheria za kimataifa hazizingatiwi kabisa.
-
Kufanyishwa kazi watoto Sudan Kusini kwafikia viwango vya kutisha
Oct 26, 2025 01:14Ripoti iliyotolewa na serikali ya Sudan Kusini kwa ushirikiano na Save the Children imefichua kwamba takriban 64% ya watoto wa Sudan Kusini wenye umri wa kati ya miaka 5 na 17 wanahusika katika aina mbaya zaidi za ajira kwa watoto, ikiwa ni pamoja na ajira ya kulazimishwa, ukatili wa kingono, wizi, na kuhusika katika migogoro ya silaha.
-
Rais wa Brazil akosoa Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kuzuia mauaji ya kimbari Gaza
Oct 26, 2025 01:13Rais wa Brazil, Luiz Inácio Lula da Silva, ameukosoa Umoja wa Mataifa na taasisi za kimataifa kwa kushindwa kuzuia mauaji ya kimbari ya Israeli dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, akiamini kwamba vyombo hivi havifanyi kazi yao ipasavyo.
-
Wamarekani milioni 42 wako hatarini kukumbwa na njaa kutokana na kufungwa shughuli za serikali
Oct 26, 2025 01:12Takriban Wamarekani milioni 42 wanakabiliwa na tishio la njaa ikiwa kufungwa kwa shughuli za Serikali ya Shirikisho kutaendelea, na iwapo ufadhili wa SNAP utasimamishwa Novemba 1.
-
Spika Berri: Umoja kati ya makundi ya Lebanon ndio msingi wa ushindi dhidi ya Israel
Oct 26, 2025 01:11Nabih Berri Spika wa Bunge la Lebanon ametaja uhusiano na umoja uliopo kati ya serikali, wananchi, jeshi na vikosi vya Muqawama kama ufunguo wa kupata ushindi wa mwisho dhidi ya utawala haramu wa Israel.