-
Ansarullah Yemen: Hakuna meli ya Saudi Arabia inayoruhusiwa kupita Lango Bahari la Bab al-Mandab
Jul 27, 2026 10:14Harakati ya Ansarullah yaYemen imesema kuwa Mlango Bahari wa Bab al-Mandab umefungwa kikamilifu kwa Saudi Arabia, huku ikisisitiza msimamo wake kuhusu hatua zinazohusiana na usalama wa njia hiyo muhimu ya baharini.
-
Baghaei: Marekani imesaliti diplomasia kwa mara ya tatu
Jul 27, 2026 09:49Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, amesema kuwa Marekani imeisaliti diplomasia kwa mara ya tatu, akieleza kuwa hatua za Washington zimeendelea kudhoofisha juhudi za kutatua migogoro kupitia mazungumzo.
-
Maambukizi ya Ebola DRC yazidi kuongezeka, yapindukia visa 3,000
Jul 27, 2026 09:47Maambukizi ya virusi vya Ebola yanaendelea kuongezeka kwa kasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
Jeshi la Sudan lasonga mbele kaskazini mwa Kordofan na kukomboa maeneo kadhaa
Jul 27, 2026 09:32Jeshi la Sudan limetangaza kuendelea kusonga mbele katika jimbo la Kordofan Kaskazini, likisema kuwa limeudhibiti mji wa Barah pamoja na miji mingine kadhaa baada ya operesheni za kijeshi dhidi ya vikosi pinzani.
-
Maelfu Waandamana Jakarta kulaani mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza
Jul 27, 2026 08:41Maandamano makubwa yamefanyika katika mji mkuuu wa Indonesia Jakarta kulaani mashambulio ya kinyama ya jeshi la utawala haramu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza.
-
Je, Marekani imefikia mkwamo wa kimkakati katika mgogoro wake na Iran?
Jul 27, 2026 07:10Wachambuzi wengi mashuhuri wa Marekani wanaonya kwamba Washington inatembea kwenye njia ya mgogoro na Iran ambayo si lazima ifanikiwe kisiasa au kistratijia. Wanaamini kwamba changamoto kuu inayoikabili Marekani kwa sasa si kuanzisha vita, bali ni kutafuta njia ya kujiondoa kwenye mkwamo unaozidi kuongezeka siku hadi siku.
-
Kiongozi Muadhamu: Uimara wa Hizbullah ni ujumbe kwa mataifa huru
Jul 27, 2026 03:59Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, ameisifu harakati ya Hizbullah kwa msimamo wake thabiti na usioyumba katika kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema, kuwa uimara wa harakati hiyo ya Lebanon ni ujumbe wenye nguvu wa ukombozi kwa mataifa yaliyodhulumiwa duniani kote.
-
Pezeshkian: Uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na Marekani ufuatiliwe kisheria kimataifa
Jul 27, 2026 03:57Rais Masoud Pezeshkian amelaani mashambulizi ya hivi karibuni ya Marekani dhidi ya miundombinu ya usafiri ya Iran akiyataja kuwa ni "uhalifu wa kivita," na kutaka hatua za kisheria za kimataifa zichukuliwe dhidi ya uharibifu uliosababishwa na nchi hiyo kwenye vituo vya mpakani, vituo vya forodha na mitandao ya usafirishaji.
-
Hamas yalaani hatua za 'Zio-American' zinazolenga UNRWA, yahimiza hatua za kimataifa
Jul 27, 2026 03:52Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani hatua mpya za Marekani na Israel zinazolenga Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), likitaka kuchukuliwe hatua za dharura za kimataifa dhidi ya kampeni ya "Wazayuni-Marekani" ya kutaka kulisambaratisha shirika hilo.
-
UN: Wanawake wa Sudan wanakabiliwa na mashambulizi wakitafuta maji
Jul 27, 2026 03:50Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women) limetangaza kwamba wanawake na wasichana katika eneo la al-Obeid nchini Sudan wanakabiliwa na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na ukatili wa kingono wanapokuwa katika jitihada za kupata maji huku hali ya kibinadamu ikizidi kuwa mbaya.