-
Mwanamuziki wa Somaliland afungwa jela bila kesi kwa kutunga wimbo wa al-Quds
Jul 12, 2026 04:13Askari usalama katika eneo lililojitenga na Somalia la Somaliland wamemkamata mwanamuziki kijana, Khalid Mohamud Abdillahi, anayejulikana sana kama Khalid Kamil, baada ya kutunga wimbo kuhusu al-Quds iliyokaliwa kwa mabavu. Hayo yameripotiwa na Hiiraan Online, ikinukuu familia yake.
-
Ushiriki wa Wamarekani kwenye mazishi ya Ayatullah Khamenei waibua hasira huko Washington
Jul 12, 2026 04:11Mazishi ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Shahidi Ayatullah Ali Khamenei, hayakuwa tukio la Iran pekee; bali pia uwepo mkubwa wa watu wenye ushawishi na wanablogu wa kigeni katika shughuli hiyo, wakiwemo Wamarekani ambao wamesema walikwenda Iran kuonyesha mshikamano wao na kutetea simulizi ya nchi hiyo mbele ya Marekani na Israel, umezusha hasira kubwa katika duru za Magharibi.
-
Ayatullah Mojtaba Khamenei asifu ushiriki ‘wa kihistoria’ wa waumini katika mazishi, aapa kulipiza kisasi kwa Kiongozi Shahidi
Jul 11, 2026 12:01Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, ametoa shukrani zake za dhati kwa mahudhurio “ya kustaajabisha, yenye kuvunja nguvu za adui na ya kihistoria” katika mazishi ya Kiongozi Shahidi, akisisitiza kuwa malipo ya kisasi dhidi ya “watenda jinai wauaji waliodhalilika” ni jambo la yakini.
-
Utawala wa Israeli wamzuia Mufti wa Palestina kuingia Msikiti wa al-Aqsa
Jul 11, 2026 11:59Utawala wa Kizayuni wa Israel umemzuia Mufti Mkuu wa Palestina kuingia katika uzio wa Msikiti wa al-Aqsa jijini Al Quds (Jerusalem) kwa muda wa wiki moja baada ya kumteka nyara, katika hatua nyingine inayolenga viongozi wa kidini wa Palestina.
-
Wanafunzi wa Iran washinda katika Olympiadi ya kimataifa ya hisabati ya China
Jul 11, 2026 11:57Makamu wa Rais wa Iran anayeshughulikia masuala ya sayansi na teknolojia amepongeza ufanisi wa timu ya taifa ya Olympiad ya Hisabati ya Iran baada ya kushinda nafasi ya kwanza katika Mashindano ya Kimataifa ya Hisabati ya China (IMSC) ya mwaka 2026. Mafanikio haya yameelezwa kuwa ni dhihirisho la uwezo wa Iran katika nyanja ya sayansi.
-
Russia na China zapinga mashinikizo ya Magharibi dhidi ya Iran katika Baraza la Usalama
Jul 11, 2026 11:31Russia na China zimepinga vikali kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) kilichochochewa na nchi za Magharibi kuhusu Iran siku ya Ijumaa, zikisisitiza kuwa Azimio namba 2231 lilifika ukingano mnamo Oktoba 2025, na hivyo Baraza hilo halina tena mamlaka ya kisheria kujadili suala la nyuklia la Tehran.
-
Maambukizi ya Ebola yapanda hadi zaidi ya 1,800 nchini DRC huku virusi vikisambaa hadi mkoa wa nne
Jul 11, 2026 11:28Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imevuka 1,800, kwa mujibu wa takwimu rasmi zilizotolewa siku ya Jumamosi, huku virusi hivyo vikisambaa hadi mkoa wa nne katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
-
Matamshi ya Waziri wa Vita wa Israel kuhusu Lebanon yana taathira gani?
Jul 11, 2026 07:49Israel Katz, Waziri wa Vita wa utawala ghasibu wa Israel, amejibu matamshi ya hivi karibuni ya Donald Trump kuhusu kuondoka Israel katika ardhi ya Lebanon kwa kuyapinga vikali, na kusema Israel haitaomba idhini ya mtu yoyote katika kuendelea kusalia nchini Lebanon.
-
Iran yaonya: Mashambulizi dhidi ya miundombinu yetu yatajibiwa kikamilifu
Jul 11, 2026 04:45Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mohammad Baqer Zolqadr, ametoa onyo kali na la moja kwa moja katika ujumbe wake kupitia mtandao wa X siku ya Ijumaa, akijibu vitisho vilivyotolewa hivi karibuni na Rais wa Marekani, Donald Trump.
-
Iran yalaani vikali mashambulizi ya kigaidi nchini Pakistan
Jul 11, 2026 04:42Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali mashambulizi ya kigaidi yaliyotikisa mkoa wa kusini-magharibi mwa Pakistan wiki hii.