-
Mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi: Ujumbe na Umuhimu Wake
Jul 08, 2026 11:36Misafara ya mazishi ya mwili wa Ayatollah Khamenei, Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi, imefanyika kwa kishindo katika mji mkuu Tehran na katika miji mitakatifu ya Qom nchini Iran, na Najaf na Karbala nchini Iraq, ikihudhuriwa na mamilioni ya watu wa nchi mbili hizi na vile vile wa nchi nyingine za eneo.
-
Jibu la Awali la Jeshi la Iran: Shabaha 85 za jeshi la Marekani zalengwa
Jul 08, 2026 04:49Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza rasmi kuwa, katika hatua ya kwanza ya kujibu uchokozi wa Marekani wa usiku wa kuamkia leo, vikosi vya wanamaji na anga vya Jeshi hilo, katika operesheni ya pamoja ya makombora na ndege zisizo na rubani (drones), vimetekeleza kwa mafanikio mashambulizi makali dhidi ya shabaha 85 muhimu vya kijeshi la Marekani na kutungua ndege moja ya kisasa ya kijasusi ya adui aina ya MQ9.
-
Rais Pezeshkian na Waziri Mkuu wa Iraq waongoza mapokezi ya mwili wa Kiongozi Shahidi mjini Najaf
Jul 08, 2026 04:49Rais Masoud Pezeshkian na Waziri Mkuu wa Iraq, Ali al-Zaidi, wamehudhuria hafla rasmi ya mapokezi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Najaf, kwa ajili ya kupokea mwili wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, kabla ya kuanza kwa taratibu za mazishi nchini Iraq.
-
Uganda kuwa mwenyeji wa Makao Makuu ya Kamisheni ya Kiswahili ya Umoja wa Afrika
Jul 08, 2026 04:47Kamisheni ya Kiswahili ya Muungano wa Afrika, (AU) kwa kifupi ACALAN-Kiswahili itajenga makao yake makuu nchini Uganda katika jitihada za kuhakikisha kuwa lugha hiyo inaimarika barani Afrika.
-
Mwenyekiti wa AU: Umoja wa Afrika wathamini uungaji Mkono wa Russia
Jul 08, 2026 04:44Umoja wa Afrika (AU) unathamini kwa dhati uungaji mkono wa Russia katika kushughulikia masuala muhimu ya bara la Afrika ndani ya baraza la Umoja wa Mataifa, na unakaribisha msimamo wa Moscow katika kuimarisha ufadhili wa vikosi vya kulinda amani barani Afrika.
-
Araghchi: Wananchi na Majeshi ya Iran hawatikisiki kwa vitisho vyovyote
Jul 08, 2026 04:39Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi, amesema kuwa mamilioni ya Wairani wamekusanyika kwa umoja kutoa heshima za mwisho kwa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, na urithi wake adhimu. Akisisitiza msimamo huo, amesema kuwa wananchi wa Iran na Majeshi ya Ulinzi hawatayumbishwa na vitisho vyovyote.
-
Eslami: Maendeleo ya Nyuklia ya Iran yanatokana na mwongozo na uungaji mkono wa Kiongozi Shahidi
Jul 08, 2026 04:34Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) anasema kuwa sekta ya nyuklia ya Jamhuri ya Kiislamu imefikia kiwango chake cha sasa cha maendeleo kupitia mwongozo na uungaji mkono thabiti wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
-
Simulizi ya Kimataifa kuhusu Nguvu ya Iran: Mazishi ya Kiongozi Shahidi Yatawala Vichwa vya Habari vya Kimataifa
Jul 07, 2026 10:29Sambamba na kufanyika msafara wa mazishi ya Ali Khamenei, Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu mjini Tehran, macho ya ulimwengu mzima yalikuwa yameelekezwa Iran. Kilichofanyika mjini Tehran hayakuwa maombolezo tu bali lilikuwa tukio la kisiasa na kihistoria lililoakisiwa pakubwa kimataifa na vyombo vya habari.
-
Mamilioni wauaga mwili wa Imam Shahidi Khamenei katika mji wa Qom
Jul 07, 2026 10:00Mamilioni ya waombolezaji leo walikusanyika katika mji mtakatifu wa Qom tangu asubuhi kushiriki katika mazishi ya Kiongozi Shahidi.
-
Rais Pezeshkian kuhudhuria mazishi ya Ayatullah Khamenei nchini Iraq
Jul 07, 2026 09:43Rais Masoud Pezeshkian wa Iran alitarajiwa kusafiri kwenda Iraq leo Jumanne kuhudhuria shughuli ya mazishi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeuawa shahidi, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, iliyopangwa kufanyika katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala kesho Jumatano.