-
Rais wa Afrika Kusini asema, mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni yameiaibisha nchi yake
Aug 16, 2026 09:50Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema, nchi yake "ina wasiwasi na aibu kubwa" kwa jinsi vikundi vya wanamgambo walivyowatendea raia wa kigeni wakati wa maandamano ya hivi karibuni ya kupinga wahamiaji yaliyowalazimisha maelfu kukimbia nchi.
-
Kiongozi wa muqawama ataka kuhitimishwa udhibiti wa moja kwa moja wa kifedha wa Marekani kwa Iraq
Aug 16, 2026 09:31Katibu Mkuu wa kundi la muqawama la Iraq la Kata’ib Sayyid al-Shuhada amekosoa vikali udhibiti wa moja kwa moja wa Marekani wa fedha na uchumi na mali za Iraq na kutaka kutafutwa masoko mbalimbali ya mauzo ya nje, kuimarisha uhusiano wa kibenki na kuhitimisha kivitendo udhibiti wa kifedha wa Washington kwa nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Muirani anyongwa kwa kuwagonga polisi wakati wa ghasia zilizofadhiliwa na wageni
Aug 16, 2026 09:17Mwanamume aliyehukumiwa kwa kuwagonga na kuwajeruhi maafisa kadhaa wa polisi wakati wa ghasia zilizoungwa mkono na kufadhiliwa na wageni kote Iran mwezi Januari, ameuawa.
-
Mkuu wa Idara ya Mahakama amwambia Trump: Iran ndiyo mmiliki na mtawala wa Lango la Hormuz
Aug 16, 2026 05:56Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran, Gholam-Hossein Mohseni-Eje’i, amezitaja kauli za hivi karibuni za Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu umiliki wa Lango Bahari la Hormuz kuwa ni "upuuzi," akisisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ndiyo mmiliki na mtawala halisi wa lango hilo.
-
Mauaji ya Kimbari: Sera Rasmi ya Wazayuni
Aug 16, 2026 05:10"Mauaji ya kimbari na ubaguzi wa rangi ni mradi rasmi wa utawala wa Israel." Kwa maneno haya, Francesca Albanese, Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, ameangazia uhalisia wa kisiasa na kisheria katika ardhi hizo.
-
UN: Ebola inaua mtu mmoja kila baada ya nusu saa huko Congo DR
Aug 16, 2026 03:17Tom Fletcher, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Kibinadamu, ametangaza kwamba mlipuko wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo sasa unaua mtu mmoja kila baada ya nusu saa, akitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka kupambana na mlipuko huo.
-
Mkuu wa Baraza la Uongozi Sudan: Jeshi liko tayari kwa amani; apinga kurejea madarakani RSF
Aug 16, 2026 03:12Mkuu wa Baraza la Uongozi la Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, amesema kuwa jeshi bado limedhamiria kuwashinda wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF)—kikosi cha kijeshi kisicho rasmi- na amesisitiza kuwa jeshi liko tayari kupokea kile alichokiita juhudi za "kweli" za amani.
-
UN: Kikomboleo cha dola milioni 50 kilichochea mashambulizi ya Al-Qaeda nchini Mali
Aug 16, 2026 03:07Umoja wa Mataifa umearifu kuwa fedha za kikomboleo takriban dola milioni 50, zilizolipwa mwishoni mwa mwaka 2025 ili kuwaachia huru mateka nchini Mali, zilisaidia kufadhili wanamgambo wenye uhusiano na mtandao wa kigaidi Al-Qaeda na hujuma zao katika eneo zima la magharibi mwa Afrika.
-
Qalibaf: Nilisitisha mazungumzo baada ya shambulio la Israel dhidi ya Dahiyeh huko Beirut
Aug 16, 2026 03:05Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kuwa alisitisha mazungumzo kufuatia shambulio la Israel dhidi ya eneo la Dahiyeh mjini Beirut nchini Lebanon, na kusema kuwa Iran itaushambulia utawala huo haraka iwezekanavyo.
-
Salman Al-Farsi; mhangaikaji wa kutafuta haki na ukweli
Aug 15, 2026 13:58Assalamu Alaykum mpenzi msikilizaji popote pale ulipo. Tarehe 31 ya mwezi wa nne wa Tir katika kalenda ya Hijria Shamsia ya Kiirani ni siku rasmi katika kalenda hiyo ya Kumuenzi Salman Al-Farsi. Kutokana na tarehe hiyo kusadifiana na Julai 22, makala yetu ya wiki kwa juma hili itaangazia kwa ufupi kisa cha maisha ya sahaba huyo mtukufu aliyeenziwa na kupewa hadhi maalumu na Bwana Mtume SAW. Kuwa pamoja nami basi kuanzia awali hadi tamati ya safari hii.