-
Mkuu wa IRGC: Iran imelipigisha magoti jeshi lenye silaha nyingi zaidi duniani
Aug 15, 2026 11:00Mkuu wa Jeshi la Walinzi mwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema kuwa, Iran imefanikiwa “kulipigisha magoti jeshi lenye silaha nyingi zaidi katika historia ya dunia”, kupitia operesheni za mashambulizi na ulinzi zilizotekelezwa kwa mafanikio licha ya mashambulizi makali ya adui.
-
Araghchi: Bado Hatujachukua uamuzi wowote wa kuanzisha upya mazungumzo na Marekani
Aug 15, 2026 10:59Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa, Tehran bado haijachukua uamuzi wowote wa kuanza tena mazungumzo na upande wa Marekani.
-
Iran yaitaka Ufaransa kutoa maelezo kuhusu mienendo “haramu” ya wanadiplomasia wake
Aug 15, 2026 10:57Wizara ya Usalama wa Taifa ya Iran imeionya Ufaransa dhidi ya kuingilia mambo ya ndani ya taifa hili, ikisema kuwa Paris inapaswa kutoa maelezo kuhusu mienendo na shughuli haramu za wanadiplomasia wake.
-
Kiongozi wa Hizbullah: Muqawama hautasalimu amri wala kurudi nyuma katika kulinda mamlaka ya Lebanon
Aug 15, 2026 10:56Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbollah amesema kuwa, Muqawama hautakubali kusalimu amri wala kurudi nyuma katika kulinda mamlaka, heshima na umoja wa ardhi ya Lebanon, akiongeza kuwa Israel na Marekani zimekuwa zikiilazimisha Beirut kutekeleza matakwa yao na kudhoofisha mamlaka ya nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Umoja wa Mataifa: Wakimbizi 650,000 Sudan Kusini hatarini kukosa chakula
Aug 15, 2026 10:54Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa zaidi ya wakimbizi 650,000 Sudan Kusini wako hatarini kukosa chakula katka wiki chache zijazo.
-
Matokeo ya Kuendelea Vita: Marekani Iliyodhoofika na Iran Iliyoimarika
Aug 15, 2026 05:46Seneta mmoja wa Marekani amekiri kuwa kuendelea vita kati ya Marekani na Iran kutapelekea Marekani kudhoofika na Iran kuimarika zaidi.
-
Iran yaonyesha mabaki ya ndege za kivita za Marekani na Israel ilizozitungua +Video
Aug 15, 2026 03:54Iran imeonyesha sehemu za vifaa vilivyopatikana kutoka ndege za kivita zisizo na rubani (droni) za Marekani na Israel, pamoja na ndege ya kivita ya F-15 ambazo zilitunguliwa kwa mifumo ya ulinzi ya Iran wakati wa vita. Mifumo ya ulinzi iliyotumika kutungua ndege hizo za adui imeundwa hapa nchini.
-
Jerusalem Post: Israel imeshtushwa na kasi ya Iran ya kujiimarisha upya kijeshi
Aug 15, 2026 03:53Gazeti la kizayuni la Jerusalem Post limefichua kuwa, maafisa wa ulinzi wa Israel wameshtushwa na namna Iran ilivyojenga upya na kwa kasi uwezo wake wa kijeshi tangu baada ya mashambulizi makali ya Marekani na utawala huo wa kizayuni wakati wa kipindi cha mwanzoni mwa vita vya kichokozi vilivyoanzishwa na tawala mbili hizo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Uturuki yaitaka Tunisia imuachie kiongozi wa chama cha Kiislamu cha Ennahda anayesota gerezani
Aug 15, 2026 03:51Spika wa Bunge la Uturuki, Numan Kurtulmus, ametoa wito wa kutaka kiongozi wa chama cha Kiislamu cha Ennahda na Spika wa zamani wa Bunge la Tunisia, Rached Ghannouchi, ambaye anaendelea kusota gerezani, apatiwe matibabu na kuachiwa kwa kuzingatiwa utu na ubinadamu.
-
Zaidi ya 70% ya Wapalestina wanapinga HAMAS kukabidhi silaha kabla Israel kuondoka kikamilifu Ghaza
Aug 15, 2026 03:49Uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa na Kituo cha Utafiti wa Sera na Utafiti cha Palestina (Palestinian Center for Policy and Survey Research) unaonyesha kuwa, zaidi ya asilimia 70 ya Wapalestina wanapinga Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina, HAMAS kukabidhi silaha zake kabla utawala wa kizayuni wa Israel kuondoka kikamilifu katika Ukanda wa Ghaza.