-
Trump: Kama nisingesimamisha vita na Iran, tungeachwa bila mafuta
Jun 20, 2026 11:47Katika mahojiano na chombo cha habari cha Marekani Axios, Rais Doland Trump wa Marekani amekiri hadharani kwamba hakuwa na budi ila kufanya mazungumzo na Iran kwa ajili ya kumaliza vita.
-
Iran yasitisha mazungumzo na Marekani nchini Uswisi baada ya Israel kuendeleza hujuma Lebanon
Jun 20, 2026 04:26Mazungumzo ya kidiplomasia kati ya Iran na Marekani nchini Uswisi, yaliyokusudiwa kuimarisha Hati ya Makubaliano (MoU) iliyosainiwa hivi karibuni, yameahirishwa.
-
IRGC: Tuko tayari kuwapa maadui ‘kichapo kikubwa zaidi’ ikiwa haki za Iran zitakiukwa
Jun 20, 2026 04:24Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limethibitisha utayari wake wa kuwapa maadui “kichapo kikubwa cha kihistoria” iwapo wataendeleza madai yao ya kupita kiasi na kukiuka haki za taifa tukufu la Iran.
-
Iran yawasilisha malalamiko FIFA kuhusu vikwazo vya Marekani kabla ya mechi na Ubelgiji
Jun 20, 2026 04:16Shirikisho la Soka la Iran limetangaza kuwa limewasilisha malalamiko rasmi kwa Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) kufuatia kukataliwa kwa mara ya pili mfululizo kwa mipango ya maandalizi ya Timu ya Taifa ya Iran, Team Melli.
-
UN: Israel imeua watoto 265 wa Kipalestina tangu Oktoba 2025
Jun 20, 2026 04:15Huku utawala katili wa Israel ukiendeleza jinai Lebanon, mashirika ya misaada ya kibinadamu yametoa tahadhari mpya kuhusu Gaza, ambapo watoto 265 wa Kipalestina wameuawa katika mashambulizi ya Israel tangu usitishaji wa mapigano ulipotangazwa mwezi Oktoba 2025.
-
China yaionya Israel dhidi ya kuzuia makubaliano ya Iran na Marekani
Jun 20, 2026 04:11China imeionya Israel dhidi ya kuzuia utekelezaji wa Mkataba wa Maelewano (MoU) kati ya Iran na Marekani, huku ikitaka pande zote kuchukua hatua za vitendo kuunga mkono amani ya kikanda na kuunda mazingira yanayofaa kwa mazungumzo yajayo.
-
Walinzi wa mpaka wa Iran na Iraq washirikiana kuandaa marasimu ya Arbaeen
Jun 19, 2026 12:35Walinzi wa mpaka wa pamoja wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Jamhuri ya Iraq wamefanya vikao vya pamoja katika mpaka wa eneo la Mehran katika mkesha wa kuanza rasmi wimbi kubwa la mazuwwar wa Muharram na Arbaeen.
-
Imam wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran: Utawala wa Marekani hauaminiki hata kidogo
Jun 19, 2026 12:27Huku akisema kuwa, nguvu ni matunda ya subira mitaani, medani ya vita na diplomasia kwa pamoja, Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesisitiza kuwa: 'Leo utawala wa Marekani hauaminiki hata kidogo.'
-
Mkataba wa Maelewano na Iran: Mwisho wa nguvu ya Dola la Marekani
Jun 19, 2026 12:25Tucker Carlson, mtangazaji na mchambuzi mashuhuri wa Marekani, amesema katika taarifa kuhusu makubaliano ya hivi karibuni kati ya Iran na Marekani kwamba makubaliano hayo yamemaliza kikamilifu nguvu, kiburi, majigambo na ubabe wa Marekani katika ngazi ya kimataifa na kuipelekea ikiri rasmi hadharani kwamba Iran ni mchezaji muhimu mwenye maamuzi huru, na kwamba hilo pekee limebadilisha kila kitu katika mtazamo wa kisiasa na kijeshi.
-
Utawala wa Kizayuni wakiri kuuawa na kujeruhiwa wanajeshi wake 22 katika mapigano ya kusini mwa Lebanon
Jun 19, 2026 12:24Jeshi la utawala wa Kizayuni limetangaza kuuawa na kujeruhiwa askari wake 22 katika mapigano ya jana Alhamisi jioni na vikosi vya muqawama vya Hizbullah ya Lebanon.