-
Polisi 10 wauawa katika shambulio kwenye kituo cha polisi Niger
Jan 27, 2026 23:01Askari polisi wasiopungua 10 wa Niger wameuawa wakati watu wenye silaha waliposhambulia kituo cha polisi kaskazini mwa nchi hiyo. Eneo la kaskazini mwa Niger limekumbwa na machafuko ya magenge ya wahalifu wenye silaha.
-
Baqaei: Kampeni ya kueneza uongo dhidi ya Iran imefichuliwa
Jan 27, 2026 10:07Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran mapema leo ameandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X, akionyesha video iliyorushwa hewani na Channel 12 ya Israel ambapo mwanamke Muisraeli anashangazwa na tangazo la picha yake akitajwa kuwa ni miongoni mwa "waliouawa" katika maandamano nchini Iran.
-
Uganda inapanga kuwaondoa wanajeshi wake katika kikosi cha kulinda amani Somalia
Jan 27, 2026 10:06Mkuu wa Majeshi ya Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amesema nchi yake inapanga kuondoa wanajeshi wake huko Somalia baada ya kuwepo huko kwa kipindi cha miaka 19.
-
Uhalali wa kisheria wa Iran kujihami dhidi ya vitisho vya Marekani
Jan 27, 2026 09:00Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lazima lieleze ukiukwaji uliofanywa na Marekani kwa uwazi na kwa majina yao halisi.
-
Waziri wa Afya wa Sudan: Watu 33,000 wameuawa katika vita vya ndani
Jan 27, 2026 08:19Waziri wa Afya wa Sudan, Dkt. Haitham Mohamed Ibrahim, ameeleza hali ya kiafya nchini Sudan baada ya miaka mitatu ya vita, akisisitiza kuwa hali imeboreka kiasi katika baadhi ya majimbo ikilinganishwa na changamoto kubwa zinazoendelea kushuhudiwa magharibi mwa Sudan na Kordofan.
-
Obama na Clinton wawahimiza Wamarekani 'kusimama' huku maandamano yakiendelea nchini Marekani
Jan 27, 2026 07:26Marais wa zamani wa Marekani, Barack Obama na Bill Clinton, wamewahimiza Wamarekani kusimama na kutetea kile walichokiita "maadili ya msingi ya Marekani" baada mawakala wa uhamiaji wa Shirikisho huko Minneapolis kumpiga risasi na kumuua muuguzi wa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), Alex Pretti.
-
Rais wa zamani wa FIFA: Msiende Marekani kutazama Kombe la Dunia kutokana na wasiwasi wa kiusalama
Jan 27, 2026 06:56Rais wa zamani wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) amewataka watazamaji wa Kombe la Dunia wasisafiri kwenda Marekani kutokana na wasiwasi wa kiusalama.
-
Katibu Mkuu wa Hizbullah asema hawatakuwa watazamaji katika uchokozi wowote dhidi ya Iran
Jan 27, 2026 03:09Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kwa kusema: "Imam Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni Faqihi wetu Mtawala na sisi hatutabaki kuwa watazamaji mbele ya uchokozi wowote utakaofanywa dhidi ya Iran".
-
Katibu Mkuu wa UN: 'Sheria ya Msituni' inachukua nafasi ya utawala wa sheria kimataifa
Jan 27, 2026 03:09Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kwamba nidhamu ya dunia inazidi kumomonyoka huku utawala wa sheria ukifutwa, na nafasi yake kuchukuliwa na kile alichokiita "sheria ya msituni."
-
Mwanamke Muisraeli ashtuka kujiona kwenye orodha ya 'waliofariki' kwenye machafuko ya Iran
Jan 27, 2026 03:08Kijana wa kike wa kiisraeli aitwaye Noya Zion ameshtuka baada ya kuona picha yake inaonyeshwa kwenye televisheni ya taifa ya Israel kama mmoja wa watu waliouawa katika maandamano nchini Iran, mkasa ambao umezidi kudhihirisha jinsi utawala huo wa kizayuni unavyosambaza habari feki na za uwongo kuhusu machafuko ya hivi karibuni nchini Iran na namna serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ilivyokabiliana nayo.