-
Mali: Mashambulizi ya anga ya jeshi yameua magaidi zaidi ya 100 katika msitu wa Soussan
Jan 27, 2026 03:08Jeshi la Mali (FAMa) limetangaza kuwa limewaua zaidi ya magaidi 100 katika mashambulizi ya anga liliyofanya kwenye eneo la msitu katikati mwa nchi siku ya Jumapili, na kuyataja mashambulio hayo kuwa ni operesheni muhimu dhidi ya magaidi katika eneo hilo.
-
Katibu Mkuu wa NATO: Ulaya 'iendelee kuota' kama inadhani inaweza kujilinda bila ya US
Jan 27, 2026 03:08Katibu Mkuu wa NATO, Mark Rutte amesema, Umoja wa Ulaya, EU bali hata Ulaya nzima haina uwezo wa kujilinda bila ya Marekani na kusisitiza kuwa, nchi wanachama zitalazimika kutumia hadi 10% ya Pato lao la Taifa kwa ajili ya shirika hilo la kijeshi, ambayo inaweza pia isitoshe.
-
Makumi ya watu wauawa DRC na magaidi wenye mfungamano na ISIS
Jan 26, 2026 23:23Wanamgambo wanaohusishwa na kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) wamewaua raia wasiopungua 22 katika kijiji kimoja katika mkoa wa Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa na viongozi wa asasi za kiraia.
-
Russia yaionya Marekani kuhusu chokochoko yoyote dhidi ya Iran
Jan 26, 2026 23:05Serikali ya Russia imeionya Marekani kuhusiana na kuanzisha chokochoko yoyote ya kijeshi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Rwanda yakiri kushirikiana na waasi wa AFC/M23
Jan 26, 2026 23:04Rwanda imekiri kwa mara ya kwanza kwamba, inashirikiana na kundi la waasi wa AFC/M23 katika harakati za kiusalama huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
Ulimwengu unasubiri siku ya ghadhabu duniani kuunga mkono wafungwa wa Kipalestina
Jan 26, 2026 23:03Kampeni za kimataifa na za haki za binadamu zimetoa wito kwa watu huru duniani kote kushiriki katika mkusanyiko mkubwa wa kimataifa tarehe 31 Januari kwa ajili ya kuwaunga mkono Wafungwa wa Kipalestina.
-
Waandamanaji wakusanyika Marekani baada ya afisa wa uhamiaji kutekeleza mauaji
Jan 26, 2026 23:03Umati wa watu umekusanyika Minneapolis, Marekani kupinga uwepo wa maafisa wa uhamiaji wa shirikisho katika jimbo hilo, baada ya kupigwa risasi na kuuawa Alex Pretti mwenye umri wa miaka 37.
-
Ugaidi wa ndani nchini Marekani na mtazamo wa undumakuwili wa Washington
Jan 26, 2026 23:02Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani ametaja aina yoyote ya uchochezi au utekelezaji wa vurugu dhidi ya serikali kuwa ni mfano wa ‘ugaidi wa ndani’.
-
Je, vyombo vya habari vinavyohasimiana na Iran vinakiuka sheria za kimataifa katika upotoshaji?
Jan 26, 2026 09:26Kadiri wimbi la fitina, vurugu na machafuko yanayohusishwa na ushawishi wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel nchini Iran lilivyozidi kupamba moto, nafasi ya vyombo vya habari hasimu katika kuchochea vitendo vya ugaidi na kukiuka wazi misingi ya sheria za kimataifa imejitokeza kwa uwazi tena.
-
Iran: Tutatoa jibu la 'kujutisha' kwa uchokozi wowote wa maadui
Jan 26, 2026 08:49Iran imeonya kwamba, Jamhuri ya Kiislamu itatoa "jibu la kujutisha" kwa kitendo chochote cha uchokozi, ikisisitiza kwamba taifa hili sasa lina uwezo mkubwa zaidi wa kijeshi kuliko hapo awali.