Jul 22, 2023 04:00 UTC
  • Bunge la Jordan lataka Sweden ihukumiwe kimataifa na kusitishwa mikataba yote na nchi hiyo

Bunge la Jordan limetoa wito wa kuhukumiwa Sweden kimataifa kutokana na hatua yake ya kuruhusu vitendo vichafu vya kuvunjiwa heshima Qur'ani tukufu kkufanyika katika ardhi ya nchi hiyo.

Sambamba na mwito huo, Wabunge wa Jordan wametaka kusitishwa mikataba yote iliyotiwa saini na nchi hiyo.

Kafiri Salwan Momika, juzi Alkhamisi alikivunjia tena heshima Kitabu Kitakatifu cha Waislamu bilioni mbili dunia kwa ulinzi kamili wa jeshi la polisi la Sweden mjini Stockholm kama ambavyo pia aliivunjia heshima bendera ya Iraq mbele ya ubalozi wa nchi hiyo mjini humo.

Serikali ya Iraq imemfukuza balozi wa Sweden mjini Baghdad kulalamikia serikali ya nchi hiyo ya Ulaya Magharibi ya kuruhusu kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu.

Bi Hayam al-Yasiri, Waziri wa Mawasiliano wa Iraq ameyapiga marufuku mashirika yote ya Sweden kufanya kazi nchini humo ikiwa ni kujibu kitendo cha nchi hiyo ya Ulaya Magharibi cha kuruhusu kuvunjiewa heshima tena Qur'ani Tukufu na bendera ya Iraq.

Serikali ya Stockholm imejifanya kukasirishwa na kuchomwa moto ubalozi wake mjini Baghdad, wakati yenyewe huko Sweden inaruhusu na kutoa ulinzi wa kijeshi kwa mtenda jinai anayekivunjia heshima na kukichoma moto Kitabu Kitakatifu cha Waislamu bilioni mbili ulimwenguni.

Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni baadhi ya nchi za Ulaya hasa za Scandinavia zimeanzisha wimbi la kuvunjia heshima matukufu ya Waislamu bila ya sababu yoyote zaidi ya chuki zao tu kwa dini hii tukufu ya Mwenyezi Mungu. 

Tags