Aug 24, 2023 02:34 UTC
  • Walowezi wa Kizayuni na mbunge wa zamani wa Israel wauvunjia heshima msikiti wa al-Aqswa

Walowezi wa Kizayuni wenye misimamo ya kufurutu ada wakiwa pamoja na Mbunge wa zamani wa Bunge la Israel wamevamia msikiti wa al-Aqswa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kulivunjia heshima eneo hilo takatifu lenye historia kongwe.

Kitendo hicho cha kuvunjia heshima msikiti wa al-Aqswa kibla cha kwanza cha Waislamu kimefanyika kwa himaya na usimamizi kamili wa polisi wa utawala huo ghasibu.

Ripoti kutokak Palestina zinasema kuwa, Yehuda Gelik, Mbunge wa zamani wa Bunge la Israel Knesset akiwa pamoja na makumi ya walowezi wa Kizayuni jana waliuvamia msikiti wa al-Aqswa na kkuuvunjia heshima.

Msikiti wa al-Aqswa unajulikana kuwa nembo kuu ya utambulisho wa Kiislamu na Kipalestina wa eneo takatifu la Quds na utawala wa Israel unajaribu kuharibu utambulisho huo, lakini kusimama imara na kuwa macho wananchi wa Palestina kumeufedhehesha utawala huo wa Kizayuni na kupelekea njama zake kushindwa.

Hii si mara ya kwanza kwa walowezi wa Kizayuni wenye misimamo mikali kuvamia msikiti wa al-Aqswa wakisaidiwa na wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wanaotenda jinai kila uchao dhidi ya ya Wapalestina.

Vitendo vya hujuma za walowezi wa Kizayuni dhidi ya msikiti wa al-Aqswa vimekithiri zaidi baada ya kuingia madarakani serikali yenye misimamo mikali ya Benjamin Netanyahu ambayo imekuwa ikionyesha chuki za wazi wazi dhidi ya Wapalestina na maeneo yao matakatifu.

Vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu huko Palestina vinafanyika katika hali ambayo, viongozi wa nchi za Kiarabu na jamii ya kimataifa wameendelea kunyamaza kimya na kutochukua hatua zozote za maana za kukabiliana na vitendo hivyo vinavyokinzana na utu na ubinadamu.

Tags