Dec 14, 2023 07:16 UTC
  • Video: Hivi ndivyo Ghaza ilivyogeuka kuwa makaburi ya Wazayuni

Brigedi za al Qassam Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS zimesambaza mkanda mpya wa video inayoonesha namna Ghaza ilivyogeuka kuwa makaburi ya wanajeshi na zana za kijeshi za Wazayuni wavamizi.

Ukiangalia vizuri utaona jinsi Wapalestina wanavyopambana kishujaa mno kama hapo shuleni ambapo katika dakika 2:48 za video, mwanamapambano wa Palestina anaserereka kwa magoti huku anashambulia. Hayo kwa kawaida hayaonekani ila kwenye filamu za sinema na michezo ya kompyuta.

Aidha wataalamu wa kijeshi wanasema kuwa, kuweza kupiga vifaru tena vikiwa kwenye mwendo wa kasi, kunataka utaalamu wa hali ya juu na mazoezi ya muda mrefu.

Mwisho wa video, Wapalestina wanakomboa eneo hilo na kuitupa chini bendera ya jeshi la Israel na kuikanyaga kwa mguu. Hiyo ni fedheha na pigo kubwa mno pengine kuliko hata la tarehe 7 Oktoba wakati ilipoanza operesheneni ya #Kimbunga_cha_al-Aqsa kwani hivi sasa Ghaza imeshashambuliwa vibaya na kila kitu kimebomolewa, lakini bado Wapalestina wanatoa vipigo vikali kwa Wazayuni.

 

Tags