Jan 15, 2024 13:49 UTC
  • Sheikh Issa Qassim: Kushiriki Bahrain katika muungano wa baharini wa Marekani dhidi ya Yemen ni

Sheikh Issa Qassim Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain ameitaja hatua ya Manama ya kushiriki katika muungano wa baharini unaoongozwa na Marekani katika Bahari ya Sham dhidi ya Yemen kuwa ni kitendo kibaya, chenye kutia uchungu na cha fedheha.

Marekani inadai kuwa muungano huo wa baharini umeundwa kwa lengo la kukabiliana na oparesheni za jeshi la Yemen katika Bahari Nyekundu (Bahari ya Sham). Hata hivyo Ufaransa, Uhispania na Italia zimethibitisha kujitoa kwenye muungano huo  na zimekataa kukabidhi meli zao za kivita kwa uongozi wa Marekani huku Bahrain ikiwa nchi pekee ya Kiarabu iliyojiunga na muungano huo unaoongozwa na Marekani dhidi ya Yemen katika Bahari Nyekundu.  

Meli ya Muungano wa Baharini wa Marekani katika Bahari Nyekundu 

Televisheni ya al Masira imetangaza kuwa, Sheikh Issa Qassim kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain ameitaja kuwa aibu hatua ya serikali ya nchi hiyo ya kujiunga na muungano huo wa Marekani kwa ajili ya kuendeleza vita huko Gaza na kusema wananchi wa Bahrain wamefedheheshwa na msimamo uliochukuliwa na serikali yao.   

Sheikh Issa Qassim ameongeza kusema kuwa: Wananchi wa Bahrain wako katika maumivu na huzuni kwa sababu hawawezi kupigana katika safu za mujahidina wa Gaza ili kuuhami Uislamu lakini watu wa Yemen waliosimama imara na wachamungu hawakusita hata kidogo kutetea haki dhidi ya batili, na wametumia nguvu na uwezo wao wote katika uwanja huo.

Tags