Apr 23, 2024 03:08 UTC
  • Ndege za kivita za jeshi la Israel zashambulia makazi ya raia Ukanda wa Gaza

Ndege za kivita za utawala haramu wa Kizayuni Israel jana zilishambulia kusini kwa Ukanda wa Gaza na kubomoa nyumba kadhaa za raia katikati mwa Gaza na shule moja katika kambi ya wakimbizi ya al Bureij.

Ndege hizo pia zilishambulia vikali kitongoji cha al Zaitun kusini mashariki mwa mji wa Gaza. Wakati huo huo utawala wa Kizayuni umeshambulia kwa mizinga kambi la wakimbizi ya al Nuseirat katikati mwa Gaza, mashariki mwa kambi ya al Maghazi na maeneo mawili ya al-Maghraqa na al-Zahra.  

Nazo boti za kivita za utawala wa Kizayuni zilishambulia kwa makombora pwani ya kati na kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Ndege za kivita za Israel pia zimewauwa shahidi Wapalestina wasiopungua 26 wakiwemo watoto 16 na wanawake 6 katika mashambulizi yaliyolenga nyumba mbili za raia huko Rafah.  

Ndege za kivita za Israel zashambulia nyumba 2 za raia na kuuwa watu 26

Wakati huo huo Wizara ya Afya ya Palestina huko Gaza imeashiria kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni na kuuliwa shahidi Wapalestina 48 usiku wa kuamkia juzi na kueleza kuwa: Hadi sasa Wapalestina zaidi ya elfu 34 wameuawa shahidi wengi wao wakiwa ni watoto na wanawake. 

Katika upande mwingine, baadhi ya walowezi wa Kizayuni jana Jumatatu waliushambulia Msikiti wa al-Aqsa wakisaidiwa na wanajeshi wa Israel.

Tags