Nov 23, 2020 04:26 UTC
  • Bunge la Iraq: Serikali inapasa kuwasilisha matokeo ya uchunguzi kuhusu mauaji ya Kamanda Suleimani

Kamisheni ya Usalama na Ulinzi ya Bunge la Iraq imeripoti kuwa inaendelea kuishinikiza serikali ya nchi hiyo ili iwasilishe haraka iwezekanavyo matokeo ya uchunguzi kuhusu mauaji ya Kamanda Luteni Jenerali Qassim Suleimani na Abu Mahdi al Muhandis.

Mahdi Taqi Amerli Mjumbe wa Kamisheni ya Usalama na Ulinzi katika Bunge la Iraq jana alieleza kuwa, serikali ya Mustafa al Kadhimi Waziri Mkuu wa nchi hiyo inapasa katika siku chache zijazo iwasilishe bungeni matokeo ya uchunguzi kuhusu faili la mauaji ya kigaidi ya Kamanda Shahidi Luteni Jenerali Qassem Suleimani Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) na Abu Mahdi al Muhandis aliyekuwa Naibu Mkuu wa Harakati ya al Hashdu Sha'abi na wanajihadi wenzao 8. 

Kamanda Qassem Suleimani na Abu Mahdi Abu Muhandes waliouliwa kigaidi na Marekani  mjini Baghdad

Amerli ameeleza kuwa, serikali  inapasa kutoa ripoti kuhusu kushiriki Marekani katika jinai ya kigaidi ya mauaji ya Kamanda Suleimani na Al Muhandis na pia kuhusu kushambuliwa makao ya al Hashdu al Sha'abi.  

Mjumbe wa Kamisheni ya Usalama na Ulinzi katika Bunge la Iraq ameongeza kuwa bunge hilo linafuatilia suala hilo kwa karibu ili lipate ripoti hizo. 

Baadhi ya wabunge wa Iraq pia huko nyuma waliwahi kuikosoa serikali ya nchi hiyo kwa kuchelewa kutangaza natija ya chunguzi zingine muhimu na kuhusu mauaji hayo tajwa yaliyotekelezwa karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad.

Tags