Jun 13, 2023 04:40 UTC
  • Jumbe za Kiislamu za Quds: Msikiti wa al Aqsa ni mstari wetu mwekundu

Ujumbe wa ngazi ya juu wa Kiislamu na jopo la maulamaa wa Baitul Muqaddas wametahadharisha kuhusu njama za utawala wa Kizayuni za kutaka kubadili mazingira ya msikiti wa al Aqsa na kusisitiza kuwa eneo hilo takatifu ni mstari wao mwekundu.

Amit Halevi mwakilishi wa chama cha Likud katika bunge la utawala wa muda wa Kizayuni (Knesset) hivi karibuni aliwasilisha mpango ambao kwa mujibu wake, msikiti wa al Aqsa eti utagawanywa kwa kuzingatia maeneo yake. Kwa mujibu wa mpango huo unaodaiwa na Halevi, Waislamu watamiliki eneo la kusini mwa msikiti huo, Wayahudi eneo la kati na la kaskazini ikiwemo Quba la al Sakhra. 

Ujumbe wa ngazi ya juu wa Kiislamu na jopo la maulamaa wa Baitul Muqaddas wametoa taarifa na kutahadharisha kuhusu hatari ya takwa hilo la Amit Halevi mwakilishi wa chama cha Likud katika (Knesset) bunge la utawala wa Kizayuni kwa ajili ya kuugawa msikiti wa al Aqsa kati ya Waislamu na Wayahudi.  

Jumbe mbili hizo aidha zimessisitiza kuhusu athari hatari za mpango huo wa Kizayuni ikiwa ni pamoja na hatari ya kuyagawa maeneo ya msikiti wa al Aqsa, kuwaruhusu Wayahudi kuingia katika maeneo yote ya msikiti na kuvunjia heshima eneo hilo takatifu.  

Taarifa hiyo ya pamoja imeongeza kuwa, mpango huo hatari utasababisha kuupoteza msikiti wa al Aqsa na kuutwisha sera za Kizayuni msikiti huo; kwa msingi huo Waarabu wote na Waislamu duniani wanaapsa kuchukua hatua madhubuti ili kulabiliana na njama hiyo ya Wazayuni. 

Kuhusiana na hili, Muhammad Hamadeh Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas katika quds inayokaliwa kwa mabavu pia amesema:Juhudi zote za Wazayuni maghasibu zinazotekelezwa kwa lengo la kubadili muundo na mazingira ya msikiti wa al Aqsa zimefeli mkabala wa mapambano na istiqama ya wananchi wa Palestina. 

Muhammad Hamadeh

 

Tags