-
Video: Brigedi 3 za Saudia zaangamizwa; mamia ya mamluki wametekwa katika mashambulizi Najran
Sep 28, 2019 23:26Msemaji wa jeshi la ulinzi la Yemen amesema kuwa brigedi tatu za kijeshi za Saudi Arabia zimeangamizwa kikamilifu baada ya askari jeshi wa Yemen huku wakiungwa mkono na makundi ya kujitolea ya wananchi walipotekeleza oparesheni kubwa ya kijeshi katika mkoa mpakani kusini mwa Saudi Arabia.
-
Kenya yatangaza kampeni kubwa ya kupambana na silaha haramu + Sauti
Sep 26, 2019 22:59Msemaji wa serikali ya Kenya amesema kuwa watatumia mkono wa chuma kukabiliana na wale wote wanaomiliki silaha haramu nchini humo. Amesema watu hao watahesabiwa ni wahalifu wenye silaha hatari kwa maisha ya raia. Seifullah Murtadha na maelezo zaidi kutoka Mombasa, Kenya.
-
SAUTI, Serikali ya Kenya yaahidi kuchukua hatua kali kufuatia mkasa wa kuporomoka kwa paa ya shule iliyoua wanafunzi
Sep 23, 2019 13:42Nchini Kenya huzuni imeendelea kutawala kufuatia kuporomoka kwa paa ya darasa ya Shule ya Precious Talent mjini Nairobi mapema Asubuhi ya leo na kusababisha maafa kwa wanafunzi wa shule hiyo.
-
SAUTI, Mvutano kati ya Kanisa Katoliki na serikali ya Burundi washtadi, CNDD yahoji iwapo kanisa hilo nalo lina mgombea?
Sep 23, 2019 13:38Vutanikuvute kati ya serikali ya Burundi na Kanisa Katoliki imeendelea kushika kasi, huku mashirika yenye mafungamano na serikali yakilikosoa kanisa hilo na kuhoji iwapo linataka kusimika mgombea wake kwenye uchaguzi wa 2020.
-
SAUTI, Huku mkutano wa CPC ukianza nchini Uganda, weledi wamekosoa vikao hivyo kuwa havina faida kwa Afrika
Sep 23, 2019 13:35Mkutano wa nchi za Jumuiya ya Madola umeanza shughuli zake mjini Kampala, Uganda kwa kuhudhuriwa na wajumbe kutoka nchi zaidi ya 40.
-
Mateso kwa Waislamu, India yapeleka wanajeshi milioni 1 na 80,000 Kashmir + Video
Sep 19, 2019 21:56Ikiwa ni katika kuendeleza ukandamizaji wake dhidi ya Waislamu wa eneo la Kashmir linalodhibitiwa na India, serikali ya New Delhi imetuma wanajeshi wengine 180 kuungana na maelfu ya wanajeshi wake wengine katika eneo hilo.
-
Membe ahimiza uhuru wa vyombo vya habari Tanzania + Sauti
Sep 19, 2019 14:01Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki nchini Tanzania Benard Membe amesema kuwa serikali inaweza kuwa dumavu endapo haitoruhusu uhuru wa vyombo vya habari. Amari Dachi na maelezo zaidi kutoka Dar es Salaam Tanzania
-
Nduli wawili wa Waislamu CAR wapandishwa kizimbani ICC + Sauti
Sep 19, 2019 13:58Wababe wawili wa kivita wa kundi la Anti-Balaka la Jamhuri ya Afrika ya Kati wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai za Kivita ICC huko Uholanzi kujibu tuhuma za jinai za kivita na zilizo dhidi ya binadamu walizozifanya nchini mwao kati ya mwaka 2013 na 2014 wakati mapigano ya ndani Jamhuri ya Afrika ya Kati yalipopamba moto. Mwandishi wetu Mosi Mwassi na maelezo zaidi…
-
Waziri, Mkuu wa Polisi Uganda walaumiwa kwa kuruhusu unyanyasaji + Sauti
Sep 17, 2019 01:52Waziri wa Usalama wa Uganda na Mkuu wa Jeshi la Polisi la nchi hiyo wanatuhumiwa kutowajibika ipasavyo katika kupambana na uvunjaji wa haki za washukiwa wa makosa mbalimbali nchini humo. Kigozi Ismail na taarifa zaidi kutoka Kampala
-
Watanzania: Wamarekani ndio waliotengeneza Ebola kuwamaliza Waafrika + Sauti
Sep 15, 2019 12:14Kufuatia uvumi wa kuibuka maradhi ya Ebola nchini Tanzania, Watanzania wengi wamekua wakieneza taarifa kwenye mitandao ya kijamii zinazoeleza kuwa, ugonjwa huo ulitengenezwa na Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) kwa lengo la kupunguza idadi ya Waafrika. Tumtegee sikio mwandishi wetu wa Dar es Salaam kwa taarifa kamili...