-
SAUTI, Uganda yavipiga kufuli vyombo 13 vya habari kwa kutangaza habari zililo kinyume na sera za serikali
May 06, 2019 11:12Serikali ya Uganda imevipiga kufuli vyombo 13 vya habari nchini humo kwa tuhuma za kutangaza habari zinazoenda kinyume na sera za serikali ya Kampala.
-
Wananchi wa Libya waandamana wakisema "Bin Salman ni adui wa Mwenyezi Mungu" + Video
May 05, 2019 03:01Wananchi wa Libya jana usiku waliandamana mbele ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Tripoli wakilaani uingiliaji wa kijeshi na kisiasa wa ukoo wa Aal Saud katika masuala ya ndani ya nchi yao huku wakipiga mayowe wakisema, Bin Salman ni adui wa Allah.
-
Ujumbe wa Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) nchini Kenya + Sauti
May 01, 2019 11:28Jamii ya wafanyakazi nchini Kenya imeitaka serikali kumaliza tatizo la ufisadi ambalo limeshika kasi sana nchini. Hayo yametolewa na wafanyakazi hao katika sherehe za Siku ya Mfanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo pamoja na mambo mengine wameitaka serikali ya Nairobi kuwaandalia mazingira salama ya kazi ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
-
Kiongozi wa Daesh adaiwa kuonekana tena baada ya kupita miaka 5 + Video
Apr 30, 2019 02:04Kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh limesambaza mkanda wa video unaodai kumuonyesha kwa mara ya kwanza, baada ya kupita miaka mitano, kiongoza wa kundi hilo Ibrahim as-Samarrai, mashuhuri kama Abubakr al-Baghdadi.
-
Ubakaji waongezeka Burundi, baadhi ya viongozi wa Kanisa watuhumiwa + Sauti
Apr 29, 2019 12:29Baadhi ya wachungaji na viongozi wa Kanisa wanatuhumiwa kujihusika na visa vya upakaji na unyanyasaji wa kijinsia vinavyozidi kuongozeka nchini Burundi licha ya kuweko juhudi kubwa za kupambana na unyanyasaji wa kingono na kijinsia nchini humo. Hamida Issa na maelezo zaidi kutoka Bujumbura.
-
Polisi mjini Kampala wapambana na vijana wenye hasira + Sauti
Apr 29, 2019 12:27Ghasia za kisiasa na kijamii zimeongezeka mjini Kampala Uganda na kuwalazimisha polisi kutumia nguvu kukabiliana na ghasia hizo. Mwandishi wetu wa Kampala Kigozi Ismail na maelezo zaidi.
-
Albino kuandamana Tanzania kulaani jinai wanazofanyiwa
Apr 28, 2019 13:28Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi (Albino) nchini Tanzania kimeazimia kufanya maandamano ya kulaani jinai wanazofanyiwa ikiwemo ufukuaji wa makaburi ya watu wenye ulemavu huo na kuondoka na viungo vyao. Uovu huo uko zaidi mkoani Mbeya. Ammar Dachi na maelezo zaidi kutoka Dar es Salaam, Tanzania...
-
Kongamano la mustakbali wa Waislamu linaloshirikisha nchi 25 laendelea Uganda + Sauti
Apr 27, 2019 02:21Kongamano kuhusu mustakbali wa vijana wa Kiislamu barani Afrika linaendelea katika mji mkuu wa Uganda Kampala. Viongozi wa Kiislamu kutoka zaidi ya nchi 25 wanashiriki mkutano huo. Mwandishi wetu wa Kampala, Kigozi Ismail ana maelezo zaidi...
-
Kimbunga cha Kenneth kufika kusini mwa Tanzania usiku wa leo, tahadhari zachukuliwa + Sauti
Apr 25, 2019 12:12Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA) imetangaza kuwa, kimbunga Kenneth kimeongezeka kasi na kinatarajiwa kufika pwani ya kusini ya Tanzania na kaskazini mwa Msumbiji kuanzia usiku wa leo. Hadi sasa wameshapokelewa watu takribani mia sita katika eneo la hifadhi. AMARI DACHI na taarifa zaidi akiripoti kutoka Dar es Salaam
-
Mahakama Kuu Rwanda yatupilia mbali mashtaka kuhusu vibonzo vinavyomuhusu Kagame + Sauti
Apr 25, 2019 12:08Mahakama Kuu nchini Rwanda imetupilia mbali mashtaka yaliyokuwa yametolewa na baadhi ya wanasheria nchini kupinga sheria iliyoanzishwa mwaka jana kuwa ni kosa la jinai kuchora vibonzo vinavyomkejeli Rais wa nchi hiyo. Wakati huo wanasheria hao walianzisha kesi kulipinga hilo huku wakisema hiyo ilikuwa ni kinyume cha katiba ya nchi hiyo. Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi